UJUMBE KWA WAISLAM DUNIANI KOTE.


 "Utukufu ni (wake) ambaye alimpeleka mja wake usiku kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Falastin) ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya dalili zetu. Hakika yeye ni mwenye kusikia, mwenye kuona." (Qur'an: 17:1)

UKOMBOZI WA FALASTIN:

Katika vita vya Khaybara, Tarekh inaonyesha kuwa: Mtume (s.a.w.w) alimpeleka kila mmoja katika Maswahaba, akampa bendera kwenda kupigana na Mayahudi, hakuna aliyeshinda. Mpaka Mtume (s.a.w.w) alipompa bendera mtu ambaye ni Mpenzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Akaenda akapigana akashinda, Khaybar ikawa mikononi mwa Waislamu. Sasa Mayahudi wamekita nguzo zao katika ardhi ya Falastin, tunawasikia kina Marhab wanajisifu na kujivuna na wanamdharau kila mtu.
Wanaendesha mauaji ya halaiki, na kuangamiza kila kitu.