Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran amesema Uislamu ndio mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu na kwamba dini hii ina historia ndefu sambamba na msingi wa kinadharia na kivitendo wa haki za binaadamu. Ayatullah Sadeq Amoli Larijani mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran ameyasema hayo leo Jumanne na kuongeza kuwa suala la haki za binaadamu ni muhimu sana katika jamii za Waislamu. Ameendelea kusema kuwa, katika Uislamu heshima na haki ya mwanaadamu ni mambo yanayopewa umuhimu mkubwa sana. Ayatullah Larijani amesema kuna umuhimu wa kukabiliana na hujuma na propaganda potofu ya Wamagharibi dhidi ya haki za binaadamu katika Uislamu. Amesema, kuutetea Uislamu mbele ya hujuma ya nchi za Magharibi ni Jihadi kubwa katika njia ya Uislamu. Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran ameashiria aya kadhaa za Qur'ani na riwaya mbalimbali kuhusiana na heshima na haki za binaadamu katika Uislamu. Ameongeza kuwa zaidi ya miaka 1400 Qur'ani Tukufu, Mtume Mtukufu SAW na Maimamu Watoharifu SA walibainisha wazi masuala ya haki za binaadamu katika Uislamu. Ayatullah Larijani ameelezea kusikitishwa kwake na namna nchi za Magharibi zinavotumia vibaya suala la haki za binaadamu dhidi ya nchi huru zenye kujitegemea ambazo zinapinga ubeberu. Amesema Wamagharibi wanajaribu kulazimisha mitazamo yao ya haki za binaadamu kwa wengine duniani katika hali ambayo kivitendo wana mitazamo ya kindumakuwili kuhusu haki za binaadamu. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/33539-uislamu,-mtetezi-halisi-wa-haki-za-binaadamu
UISLAMU, MTETEZI HALISI WA HAKI ZA BINAADAMU.