Spika wa Majlisi ya Kiislamu ya Iran (bunge) Ali Larijani amelaani vikali hatua ya Umoja wa Ulaya kuliwekea vikwazo tawi la kijeshi la harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kusema nchi hizo 28 za Ulaya zinafuata kibubusa sera za Marekani.
Akizungumza Jumatano bungeni, Larijani alisema wabunge wa Iran wanalaani vikali hatua hiyo ya kuchukiza ya Umoja wa Ulaya na kuitaja kuwa ni ya kisiasa. Ikumbukwe kuwa Julai 22, chini ya mashinikizo ya Marekani na utawala haramu wa Israel, Umoja wa Ulaya uliamua kuliwekea vikwazo tawi la kijeshi la Hizbullah.
Spika wa Majlisi ya Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono kikamilifu harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Larijani ameongeza kuwa uamuzi wa Umoja wa Ulaya unatokana na kuwa Hizbullah imekuwa ikiwalinda watu wa Lebanon ambao wanakabiliwa na uhasama mkubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Larijani aliashiria ushindi wa Hizbullah dhidi ya Israel katika vita vya siku 33 mwaka 2006 na kusema, ushindi kama huo umezitia wasi wasi nchi za Magharibi. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/33559-eu-inaifuata-marekani-kibubusa-katika-vikwazo-vya-hizbullah