Askari wa usalama nchini Lebanon, wamemtia mbaroni mtu wa karibu sana na Ahmad Al-Asir, sheikh wa Kiwahabi mwenye misimamo mikali nchini humo. askari hao wamesema kuwa, mtu huyo ni Abdul-Wahid mwenye umri wa miaka 30 na alikuwa akishirikiana kwa pamoja na Al-Asir kwa miaka kadhaa huku akiwa mtu wake wa karibu. Abdul-Wahid, ametiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa mjini Bairut, akiwa na lengo la kutoroka. Mwezi uliopita Al-Asir ambaye amekuwa mashuhuri kwa jina la sheikh wa fitina huko kusini mwa Lebanon, alianzisha vita dhidi ya jeshi la nchi hiyo na kupelekea watu zaidi ya 21 kuuawa na wengine kujeruhiwa. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amesisitiza kuwa, serikali mpya ya nchi hiyo itaishirikisha pia Harakati ya Hizbullah. Akiashiria baadhi ya njama za baadhi ya mirengo, za kutaka kuitenga harakati hiyo katika muundo wa serikali mpya, Adnan Mansour amesema, suala la kutengwa Hizbullah katika serikali mpya chini ya uongozi wa Tammam Salam, haliwezekani na ni kwenda kinyume na matakwa ya kijamii ya nchi hiyo. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/33585-mpambe-wa-sheikh-asir-akamatwa-lebanon
MPAMBE WA SHEIKH ASIR AKAMATWA LEBANON.