Maulana Sheikh Hemed Jalala,
akimkaribisha
Mwenyekiti wa Ibntv, katika Semina ya Quds iliyofanyika Masjid
Al-Ghadiir Kigogo Post, kwa ajili ya kuangalia jinsi gani wataweza
kufikisha ujumbe wa Quds katika Jamii ya Kitanzania.
Sheikh Baswalehe
amesema katika Semina ya Quds iliyofanyika Masjid Al-Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, kuwa siku ya Quds imeanzishwa na Mwanachuoni mkubwa wa Kiislam (Imam Khomein) kwa ajili ya Waislam wajitambue kwamba Quds ni yao, na kama hawataungana pamoja kutafuta njia za kuikomboa mikononi Mwamazayuni Quds itaondoka mikononi kwa Waislam, ameendelea kwa kusema atakama tunatofautiana Kimadhehebu, lakini kuna mambo ambayo yanatuweka tuwe wa moja, kwa hiyo kudai Quds ni jambo la kila Muislam, bila ya kujali tofauti zetu tulizokuwanazo, Waislam wanatakiwa waungane na wajue kuwa wanawajibu wa kuikomboa Quds kutoka katika mikono ya Mazayuni, amemalizia kwa kusema kuwa Quds ni muhimu sana kwa Waislm kwa kuwa ni moja ya Matukufu ya Waislam ambayo yanatakiwa yalindwe.
Maimamu wa Misikiti mbalimbali wakiwa katika
Semina ya Quds iliyofanyika leo Masjid Al-Ghadiir Kigogo Post, jijini
Dar es Salaam, kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa Waislam juu ya suala la
Quds.
Vijana kutoka nchi ya Jamuhuri ya Kiislam ya Iran wakisoma Nasheed katika Semina ya Quds, Masjid Al-Ghadiir Kigogo Post.