AYATULLAH KASHANI: WAMISRI WAWE MACHO MBELE YA ADUI.


Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran amewataka wananchi wa Misri kuwa macho katika kukabiliana na njama za maadui wa nchi hiyo.

Akizungumzia machafuko yanayoendelea nchini Misri, Ayatullah Muhammad Emami Kashani amesema kuwa, Misri ni moja kati ya nchi zenye ustaarabu, utamaduni, elimu, na maarifa makubwa ya Kiislamu ulimwenguni na kusisitiza kuwa, wananchi wa Misri wamekulia kwenye mafundisho ya Kiislamu ingawa leo hii maadui wameitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko. Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, ijapokuwa wananchi wa Misri hawana kiongozi mwadilifu na faqihi, lakini wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Ayatullah Kashani amewapongeza Waislamu kote duniani kwa kuingia katika ugeni wa Mwenyezi Mungu kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na kuwataka wazidi kumcha Allah katika mwezi huu. Khabari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/33283-ayatullah-kashani-wamisri-wawe-macho-mbele-ya-adui