MAFANIKIO YA KIROHO.

Mabadiliko yalikuwa ndiyo mwanzo wa mafanikio ya kiroho, kwani nilihisi raha ya nafsi na ukunjufu wa Moyo kuyaendea Madhihabu ya Haki niliyoyangundua au unaweza kusema kuwa "UISLAM HALISI AMBAO HAUNA SHAKA NDANI YAKE." Furaha kubwa na fahari vilinifunika kutokana na neema aliyonineemesha Mwenyezi Mungu kwa Uongofu na mwongozo. Sitoweza kunyamaza na kuficha yale yote yaliyokuwa yakinikeleketa kifuani mwangu, "Inanibidi niudhihirishe ukweli huu kwa watu kwani neema ya Mola wako isimulie," Nayo ni miongoni mwa neema kubwa, au ni neema kubwa mno duniani na Akhera na yeyote anayenyamazia haki ni Shetani bubu. Na hakuna kingine baada ya Haki isipokuwa ni Upotofu.

Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: "Yeyote atakayefurahishwa kuishi maisha (niliyoishi) mimi na kufa kama kifo changu na kuishi ndani ya Pepo ya milele, basi amtawalishe Ali baada yangu mimi, na (pia) amtawalishe aliyetawalishwa naye, na afuate nyayo za Ahlul-Bayt wangu baada yangu kwani wao ni kizazi changu. Wameumbwa kwa udongo nilioumbiwa mimi, na wamepewa fahamu yangu na elimu yangu. Ole wao wenye kupinga ubora wao katika Umati wangu, wenye kukata maungano yao kwangu, basi Mwenyezi Mungu asiwape Shufaa yangu."
_______________________________________________
Rejea: Tarikh Ibn Asakir J. 2 Uk. 95
Kanzul - Ummal J. 6 Uk. 155