UJUMBE

Kuchangua kitu kilicho kizuri zaidi kunapendwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu (basi wabashirie waja wangu *Ambao husikiliza kauli (nyingi zinazo semwa) kisha wakafuata zilizo nzuri zaidi), 1 na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwaamuru kuchukua kilichokuwa bora (na uwaamrishe watu wako washike yaliyo bora katika hayo), 2 na anaamrisha kauli iliyo njema (Na waambie waja wangu waseme yaliyo bora), 3 na anaamuru kufanya Mijadala katika mahala peke-kwa yale yaliyo mazuri (Na ujadiliane nao kwa yale yaliyo bora). 4
Na pindi inapo lazimika kujikinga na kujibu, anaamuru kujibu kwa yaliyo mazuri (Ondosha mabaya kwa mema), 5 na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu analipa kwa yaliyo mazuri zaidi (na bila shaka tutawapa malipo yao kwa sababu ya matendo bora waliyokuwa wakitenda), 6 na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu ameyateremsha mazungumzo yaliyo mazuri sana (Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa). 7
_______________________
1- Suuratuz-Zumar aya 18
2- Suuratul-aarafu aya 145
3- Suuratul-israa'l aya 53
4- Suuratun-nhli aya 125
5- Suuratul-muuminuun aya 96
6- Suuratun-nhil aya 97
7- Suuratuz-zumar aya 23