Makundi ya kigaidi na kisalafi nchini Iraq katika siku za hivi karibuni yameshadidisha mashambulio yao dhidi ya Waislamu wa Kisuni na Kishia nchini humo. Hivi sasa, hakuna siku inayopita bila ya kushuhudiwa kuongezeka idadi ya wahanga wa mashambulio hayo ya kigaidi nchini humo. Oparesheni za kigaidi zinaonekana kuwa endelefu nchin humo. Kwani jana ilitokea miripuko kwenye maeneo mbalimbali, na kusababisha makumi ya watu kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa. Vyombo vya usalama na hospitali nchini Iraq vinasema kuwa, kwa akali watu 70 wameuawa na wengine zaidi ya 230 kujeruhiwa katika miripuko iliyotokea jana katika maeneo mbalimbali nchini humo. Mashambulio hayo ya kigaidi yanashuhudiwa nchini Iraq katika hali ambayo, serikali ya Baghdad inayoongozwa na Nouri al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq iko mbioni kuleta umoja wa kitaifa nchini humo. Safari ya al Maliki huko Arbil na kukutana na Masoud Barazani Mkuu wa eneo la Kurdistan la Iraq, ilikuwa harakati chanya iliyofanyika kwa shabaha ya kupunguza mivutano ya kisiasa nchini humo. Amma sambamba na kufanyika safari hiyo, nchi hiyo imeshuhudia ikitumbukia kwenye wimbi kubwa la milipuko ya mabomu na machafuko. Hii ni dalili tosha inayoonyesha kuwa, maadui wa nchi hiyo hawataki kuona amani na utulivu ukirejea nchini Iraq. Makundi ya kigaidi, Kisalafi na lile la Baath hayo yote yanatumiwa kama wenzo wa kuleta ghasia na machafuko nchini humo. Swali la kujiuliza hapa ni hili kwamba, makundi yanayofanya operesheni za kigaidi nchini Iraq yana malengo gani? Je, malengo yao ni kuleta fitina za kikabila? Au ni kuandaa mazingira ya kuigawa nchi hiyo? Vyombo vya kupasha habari vya Magharibi hivi karibuni viliandika kuwa, Iraq inakaribia kutumbukia kwenye mgogoro wa kikabila na kimadhehebu. Vyombo hivyo vinaamini kuwa, mgogoro wa kisiasa wa Iraq unafungamana na baadhi ya madola ya Kiarabu ya eneo la Mashariki ya Kati, na wanataka kuwapambanisha Waislamu wa Kishia na Kisuni, ili serikali ya Nouri al Maliki ionekane dhaifu na ionekane imeshindwa kuleta amani nchini humo. Amma kwa upande mwingine, wako watu wanaoamini kwamba hivi sasa kuna mikakati maalumu imepangwa ya kutaka kuigawa nchi hiyo. Joe Biden Makamu wa Rais wa Marekani amewasilisha mkakati mbele ya viongozi wa Marekani wenye lengo la kuigawa Iraq. Hapana shaka kuwa, mkakati huo wa Washington unahusika moja kwa moja na wimbi la ghasia na machafuko nchini humo. Bila shaka, jambo lisiloweza kukanushika ni hili kwamba, machafuko na oparesheni za kigaidi zinazofanyika nchini Iraq zina mafungamano ya moja kwa moja na matukio yanayoendelea hivi sasa katika eneo hili la Mashariki ya Kati. Na hasa ikizingatiwa kuwa, hivi sasa Masalafi wanaendesha oparesheni za kigaidi nchini Syria na Lebanon. Tukiangalia upande wa pili wa matukio ya Iraq tunaweza kuona wazi kuwa, machafuko ya Iraq ni mikakati iliyopangwa na madola ya kigeni, inayotekelezwa na vibaraka wao walioko ndani ya nchi hiyo. Jambo hilo linatiliwa nguvu pale, Nouri al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq aliposema kuwa, baadhi ya nchi za eneo hili ndizo zinazohusika moja kwa moja na ghasia na machafuko nchini humo. Ijapokuwa mara zote amekuwa akikwepa kuzitaja nchi hizo hadharani, lakini bila ya shaka al Maliki amekuwa akizilenga nchi kama Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu hasa kwa kuzingatia kwamba makumi ya magaidi waliotiwa mbaroni nchini humo wana uraia wa nchi hizo. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/
MAGAIDI WAENDELEA KUUA WAISLAM WA KISUNNI NA KISHIA IRAQ.