Katibu wa Jumuhiya ya Mashia Ithna Ashariya wa Chanika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bwana Juma S. Magambilwa amesema, kabla ya mwaka 2004, Chanika hajapata taarifa kama kuli kuwa na mfuasi yeyote wa Madhehebu ya Shia katika eneo hilo, ameendelea kwa kusema mnamo mwaka huo huo (2004), mmoja katika wafusi wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariya, aliamia Chanika na familia yake ikawa ndio tone la Ushia katika bahari iliyogubikwa na Usunni hususani Uwahhab. Kwa uzoefu wake akawa hafanyi Tabligh ya wazi kwa kuchelea Bughudha za Mawahhab.
(1) Akaamua kuwashauri baadhi ya Mashia waliyopo mjini wahamie Chanika ili kujirahisishia namna ya kumiliki makazi ambapo kwa Chanika inawezekana hata kwa mtu mwenye kipato cha kawaida.
(2) Familia zisizo zidi mbili zikahamia mwishoni mwa mwaka 2008 sanjari na kuanzisha Madrasa Al Hussan Mujitaba (a.s), Madrasa hiyo ilianzishwa katika uwanja wa Mzee Upunda aliyependa Qur'anTukufu isomeshwe kwa wakazi wa Chanika, kwani yeye hana taarifa yoyote juu ya Madhehebu.
(3) Baada ya mwaka mmoja mwenyeji wetu (mshia mtangulia) aliamua kukata eneo la kiwanja chake na kuikabidhi Al Hassan Mujitaba (a.s), ijenge Madrasa.
CHANGAMOTO:-
(a) Kupoteza wanafunzi kwani tayali Mawahhab wamesha eneza sumu dhidi ya Ushia.
(b) Kukosa Mwalimu wa kufundisha kwani kwa miaka yote hiyo Mwalimu anayesimami Madrasa hiyo ni Mama wa familia.
(c) Kukosa msaada wa kujengewa Madrasa katika eneo letu kwa miaka yote hiyo. Ingawa tumejitahidi na kusimamisha Banda lililogharimu kiasi cha Shilingi Laki sita kwa nguvu zetu wenyewe.
Hii ni baada ya kuona kwamba tumesema na watu mbalimbali ambao tuna uhakika kuwa wanaweza kutupatia msaada lakini linapokuja suala la kutujengea wanaingia ukakasi. kutokana na hilo uzowefu ukatuonyesha kuwa hatusaidiwi kwa sababu zifuatazo:
(1) Wafadhili wametapeliwa sana, hivyo basi ikiwa wameumwa na Nyoka wakiona unyasi wanashituka.
(2) Namna yetu ya kuomba msaada sio hile ya kuweka mikono nyuma na hatutaiweka nyuma Abadani.
Kwa nini?
Ni kwa sababu sisi tunaamini kuwa tunapokuhamasisha kujenga Madrasa, Msikiti na kadharika manufaa yanayopatikana ni yako mwenyewe.
"Ni wewe wewe utakae jengewa majumba ya Fedha na Allah (s.w). Basi kama ni kunyenyekea, ni wewe tuliyekupa njia hiyo nzuri. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia No: 0712 147 889.