Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema uchaguzi wa rais wa Iran uliofanyika Ijumaa Juni 14 uliwavunja moyo maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqi ameongeza kuwa kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika uchaguzi wa rais ni jambo ambalo limethibitisha kuwa ya uongo madai ya maadui kuwa Wairani hawangeshiriki katika uchaguzi. Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa Tehran ameongeza kuwa maadui walitumia mbinu hatari sana kuibua fitina katika uchaguzi wa mwaka 2009 lakini mara hii wamefeli kabisa katika njama zao kutokana na kujitokeza kihamasa wananchi wa Iran katika masanduku ya kupigia kura.
Sheikh Kadhim Sidiqqi ameashiria tukio la kuuawa shahidi Ayatullah Muhammad Beheshti na makada 72 wa Mapinduzi ya Kiislamu Juni 28 mwaka 1981 na kusema tukio hilo lilitoa pigo kwa mfumo wa Kiislamu wa Iran. Sheikh Sidiqqi pia amelaani hujuma ya Mawahabbi dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Misri ambapo mwanazuoni maarufu Sheikh Hassan Shihata na wenzake watatu waliuawa shahidi. Amesema jinai hiyo inaonyesha waliotenda kitendo hicho ni makatili na majahili. Ameongeza kuwa tukio hilo la kusikitisha linapaswa kuwa kengele ya hatari kwa ulimwengu wa Kiislamu. Khatibu wa Sala ya Ijumaa amesema pote la Masalafi au Mawahabbi ni pote ambalo limeibuliwa na madola ya kibeberu duniani ili kutoa taswira potofu ya Uislamu. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/32967-uchaguzi-iran-ulivunja-moyo-wa-maadui