Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa, hivi sasa maadui wa Magharibi wameshika upanga dhidi ya Waislamu, hivyo umma wa Kiislamu unatakiwa uimarishe ngome na uwezo wake wa ndani. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliyasema hayo jana asubuhi alipoonana na wahadhiri, maqarii na mahafidh wa Qur'ani Tukufu walioshiriki kwenye Mashindano ya Thelathini ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyomalizika juzi hapa mjini Tehran na kutaja moja ya mafundisho makubwa ya Qur'ani Tukufu kuwa ni kuwataka Waislamu walinde umoja, mshikamano, mapenzi na ushirikiano baina yao. Aidha Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, hii leo kila koo na ulimi ambao unawalingania Waislamu kwenye umoja na mshikamano, koo hiyo ni ya Mwenyezi Mungu na ulimi wowote unaolingania uadui kati ya Waislamu na kati ya madhehebu za Kiislamu, ni ulimi wa shetani. Amesema kuwa, moja ya balaa ambazo hivi sasa zimeukumba ulimwengu wa Kiislamu, ni tofauti za kimadhehebu kati ya Waislamu suala ambalo amesema limesababisha kuzuka mapigano makali na umwagaji damu kati ya Waislamu wenyewe kwa wenyeweo. Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa, hii leo makundi yenye misimamo mikali isiyokubaliwa na dini tukufu ya Kiislamu, yanaendesha vitendo vya taasubi, ukatili wa kutisha, kuzusha mapigano na mienendo mingine mibaya katika nchi za Kiislamu huko barani Afrika na Mashariki ya Kati. Amesema makundi hayo yenye kuwakufurisha Waislamu wenzao licha ya kwamba yanajinasibisha na dini tukufu ya Kiislamu, yanapelekea maadui kuyatumia vibaya kwa lengo la kuupaka matope Uislamu wakati dini hii ya Mwenyezi Mungu ni dini ya kuhurumiana na kupendana huku Mtume Muhammad (SAW) akiwa mbeba bendera ya ujumbe wa mapenzi, usalama na urafiki kwa wanadamu na vioumbe wote. Ameongeza kuwa, mpasuko unaoonekana leo katika umma wa Kiislamu, ni natija ya kujiweka mbali na mizani ya ukweli na chimbuko la dini hii tukufu iliyojengeka juu ya mafundisho ya Kitabu cha Mbinguni yaani Qur'ani Tukufu. Aidha Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, ikiwa Waislamu watashikamana na Qur'ani Tukufu na mafundisho mema ya dini ya Uislamu na wakafahamu vyema ujumbe wa dini hii ya upole na mapenzi, basi wataujua vizuri udharura wa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kuachana na utengano baina yao. Amehoji kwa kusema, inakuwaje Mwislamu ajidai kumtetea Mtume Mtukufu, ilihali mikono yake imetapakaa damu za watu wasio na hatia? Amesema mienendo hiyo mibaya na isiyo ya kibinaadamu inafanyika kwa sababu ya taasubi za kijahiliya ambazo zinatokana na njama za ukoloni na lengo lake ni kuzusha tofauti za kimadhehebu na kusambaratisha umoja wa Waislamu kwa manufaa ya maadui wa umma huu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, katika hali ambayo ulimwengu wa leo unatawaliwa kwa nguvu za kisiasa na tawala za kibepari, maisha ya mwanadamu yana kiu kubwa na mafundisho asili ya Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW), wito wa Qur'ani Tukufu, uadilifu, kujitegemea, uhuru na heshima. Kujiweka mbali na mafundisho hayo ya Mwenyezi Mungu, kumesababisha maadui wa Uislamu kuzusha vita vya kila aina katika safu ya Waislamu na vile vile kueneza chuki dhidi ya Uislamu duniani. Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei pia amesisitiza katika mkutano huo juu ya ulazima kwa Waislamu kuzidi kuwa na ukuruba na mapenzi makubwa kwa Qur'ani Tukufu na kuzidi kuwafundisha Waislamu wengine mafundisho yaliyojaa uongofu na ufanisi ya Kitabu hicho Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
SISITIZO LA KIONGOZI MUADHAMU JUU YA UMOJA NA MAAFIANO YA WAISLAM.