PANAHIYAN: MATATIZO YA KIMAISHA YATATULIWE KWA FIKRA ZA KIMAPINDUZI.


Hujjatul Islam Ali Ridha Panahiyan mhadhiri wa hauza na chuo kikuu amesema kuwa, matatizo ya kimaisha na kiuchumi ya wananchi hayawezi kutatuliwa kwa njia nyingine isipokuwa fikra za kimapinduzi. Panahiyan amesema hayo akimfanyia kampeni Saeed Jalili mgombea wa uchaguzi wa rais wa Iran alipokuwa akiongea na wanafunzi wa kidini. Panahiyan ameongeza kuwa, kwa bahati mbaya kuishi kimapinduzi hata baada ya miaka kadhaa tangu ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu bado hakujaarifishwa ipasavyo na kutumika katika jamii. Aidha alimu huyo amebainisha kuwa, kuishi kimapinduzi kuna tafsiri tofauti kama vile kuimarishwa muqawama, uadilifu, maisha yenye nishati, utulivu, maendeleo na kadhalika na kwamba suala hilo linapaswa kuhuishwa kwenye jamii.
Uchaguzi wa rais wa Iran utafanyika Ijumaa ya terehe 14 Juni pamoja na uchaguzi wa Mabaraza ya Kiislamu ya Miji na Vijiji nchi nzima. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/uchaguzi-iran-1392/item/32387-pnahiyan,-matatizo,-fikra,-kimapinduzi