KUMBUKUMBU YA MWASISI WA JAMUHRI YA KIISLAM YA IRAN.

Imam Khomeini wakati wa uhai wake alikuwa akisoma na kufuatilia habari na ripoti muhimu Magazetini na kutoka  katika majarida mbalimbali ya habari, huku akiwa akifuatilia habari kupitia vituo vya Radio na Luninga vya Iran na bila kusahau Uchambuzi wa habari kupitia vyombo vya habari vya nchi za nje.
Imam Khomeini alikuwa akiamini dharura ya kuwepo mapigano, ratiba na udhibiti wa nafsi katika maisha, hivyo alikuwa akitenga muda maalumu usiku na mchana kwa ajili ya ibada, dua, na kisomo cha Qur'an. Pia alikuwa akishiriki mazoezi ya kutembea huku akimtaja Mwenyezi Mungu na kufikiria Mustakbali, kiasi kwamba alifanya kufikiria Mustakbali ni sehemu ya ratiba yake ya kila siku.
Pamoja na kuwa na kazi nyingi na mikutano ya mara kwa mara na Viongozi wa utawala wa Kiislam lakini suala la kukutana na watu wa kawaida alilipa umuhimu wa pekee, hivyo aliendelea na ratiba yake ya kila wiki ya kukutana na familia za Mashahidi hadi siku za mwisho za maisha yake.
Miaka mingi Imam Khomeini alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo, hivyo mwaka 1979 alipelekwa hospitali ya Ugonjwa wa moyo Tehran kwa ajili ya matibabu, hila sababu hasa iliyokuwa chanzo cha kifo chake ni ugonjwa uliyopatikana katika mfumo wa chakula hivyo alilazimika kufanyiwa upasuaji.
Imam Khomeini alifariki dunia saa nne na dakika ishirini siku ya J.mossi usiku sawa na Tarehe 3/6/1989, ikiwa ni baada ya kukaa hospitali muda wa siku kumi.
Ilipofika tarehe 5/6/1989 uliwekwa mwili wake uliyotakasika kwenye kiwanja kikubwa cha kusali kilichopo Tehran ili Ummah wa Wairani uweze kumuaga. Kisha mwili wake uliyotakasika ulisindikizwa na msafara wa watu wasiopungua Milioni kumi wakiwa wamevaa na kujifunika mavazi meusi huku wakimwaga machozi na kutoa sauti za kuishiwa nguvu kutokana na hasara waliyoipata ya kuondokewa na mtu mkubwa na kiongozi shupavu.