AYATULLAHIL UDHMA KHAMENEI WAIRAN WANAJIAMINI.


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amehutubia hadhara kubwa ya wananchi na wageni kutoka mataifa mbalimbali waliokuja hapa nchini kushiriki kwenye maadhimisho ya kukumbuka kutimia miaka 24 tokea alipofariki dunia Imam Khomeini MA na kusema kuwa, kujiamini na ushujaa ndio siri ya mafanikio ya wananchi wa Iran. Ayatullahil Udhma Ali Khamenei amesema kuwa, maadui waliwaelezea wananchi wa Iran kuwa ni watu wasio na uwezo kwani wako nyuma miaka 100 kwenye medani za kisiasa, kielimu na kiuchumi lakini Imam Khomeini aliwaambia wananchi wa Iran kuwa munaweza kupiga hatua kubwa kwenye medani hizo mtakapokuwa mumejenga moyo wa ushujaa na kujiamini. Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, pamoja na kuwepo njama zote za maadui lakini wananchi wa Iran wameweza kupata ushindi kwenye medani zote, na hivi sasa Iran iko huru na wala haitegemei madola ya kibeberu. Ayatullah Khamenei amesema hivi sasa Iran ni moja kati ya nchi zilizopiga hatua kielimu duniani na kusisitiza kwamba Kituo cha Utafiti Duniani kimetangaza kuwa, ukuaji wa kielimu nchini ni mkubwa na hadi kufikia mwaka 2017 Iran itashika nafasi ya nne kielimu duniani. Kuhusiana na uchaguzi wa rais hapa nchini, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, uchaguzi ni dhihirisho la hamasa ya kisiasa ya wananchi na kusisitiza kuwa, wananchi wa Iran daima wako mstari wa mbele katika uwanja wa kulinda thamani za mapinduzi. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/kiongozi/item/32399-ayatullahil-udhma-khamenei-wairani-wanajiamini