Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, muqawama ndio umepelekea kuhifadhiwa kujitawala nchi ya Lebanon, na kukomesha uchu na uporaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Akizungumza kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya majeruhi wa vita na muqawama wa Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, kama usingelikuwepo muqawama, leo hii Lebanon ingelikuwa chini ya himaya ya utawala wa Israel. Sayyid Nasrullah amesema kuwa, muqawama licha ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yakikaliwa na mabavu na majeshi ya Israel, umesababisha wananchi wa Lebanon kuwa na uhuru, utukufu na izza. Akizungumzia njama za maadui wa ndani na nje za kutaka kuisambaratisha muqawama nchini Lebanon, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa moja kati ya majeshi yenye nguvu kubwa mno katika historia, limeweza kusalimu amri mbele ya wanamapambano shupavu wa Hizbullah. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/32661-nasrullah-muqawama-utaendelea-nchini-lebanon
NASRULLAH: MUQAWAMA UTAENDELEA NCHINI LEBANON.