ASHINDANO YA 30 YA QUR'ANI TUKUFU YAANZA TEHRAN.


Mashindano ya 30 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza rasmi leo hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 70 duniani. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA), katika siku ya kwanza ya mashindano hayo baadhi ya wasomaji maarufu Qur'ani Tukufu wa kimataifa wamepewa fursa ya kusoma kwenye ufunguzi wa hafla hiyo. Mtu wa kwanza aliyepewa fursa ya kusoma Qur'ani kwenye mashindano hayo ni Muhammad Mashmol mshindi wa pili wa mashindano ya 25 ya Qur'ani Tukufu nchini Iran.

Ufunguzi wa mashindano hayo ulifanywa jana Ijumaa na Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammadi Golpaygani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi na wananchi wa Iran. Mashindano hayo yatamalizika Ijumaa tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa Siku ya Mabaath. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/32326-mashindano-ya-30-ya-qur-ani-tukufu-yaanza-tehran