HASSAN ROHANI: VIKWAZO DHIDI YA IRAN SI HALALI.


Mgombea wa duru ya 11 ya uchaguzi wa rais wa Iran Hassan Rohani amesema kwamba, vikwazo dhidi ya Iran vinavyochochewa na Marekani ni kinyume cha sheria kwani nchi za Magharibi kwa miaka 9 sasa zinatambua kuwa mipango ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo ya amani. Akizungumza kupitia televisheni ya taifa Rohani amesema, Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa ya Nishati ya Atomiki IAEA Novemba 2004 kwa sauti moja ilithibitisha kwamba mipango ya atomiki ya Iran ni kwa ajili ya malengo ya kiraia. 

Mgombea huyo wa urais wa Iran aidha amesema, Marekani tangu ilipoanza kudai kwamba Iran inataka kutengeneza bomu la nyuklia, imethibitika kuwa madai hayo ni ya uongo kwani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza wazi kwamba, kutengeneza bomu la nyuklia ni dhambi kubwa. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/uchaguzi-iran-1392/item/32240-hassan,-rohani,-vikwazo,-iran,-halali,-marekani