WANANCHI WATATHIBITISHA MAFANIKIO YA MFUMO.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi na kwa shauku taifa la Iran katika uchaguzi wa Juni 14 mwaka huu kutaonesha mafanikio makubwa ya Mapinduzi na mfumo wa Kiislamu wa Iran. Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo katika sherehe za kuhitimu wanafunzi wa chuo kikuu cha kijeshi cha Imam Hussein (A.S) hapa mjini Tehran. Huku akiwahusia wananchi kuzingatia nara na ilani za uchaguzi za wagombea ili kutambua na kumchagua yule anayefaa, Ayatullah Khamenei amesema, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mustakbali wa nchi na taifa la Iran utakuwa wazi, wenye izza na mfano kwa wote. Pia amewausia wagombea wa duru ya 11 ya uchaguzi wa rais wa Iran kujiepusha na kampeni za uharibufu na pia kuzingatia maadili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kuhudhuria kwa wingi wananchi katika vituo vya kupigia kura kunakodhihirisha ushiriki mkubwa wa taifa la Iran katika matukio mbalimbali ya nchi, bila shaka kutaandaa mazingira ya kuipatia izza na kinga serikali kimataifa, kuwafurahisha marafiki na kuwachukiza maadui wa Iran. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/32186-kiongozi-muadhamu,-ali-khamenei,-uchaguzi,-rais,-mafanikio,-jamhuri-ya-kiislamu,-iran,-wagombea