RIPOTI: HUENDA MFALME WA SAUDIA AMEFARIKI DUNIA.


Gazeti la Asharq al-Awsat linalochapishwa mjini London limeripoti kuwa Mfalme Abdullah bin Abdul-aziz wa Saudi Arabia anapumua kwa kutumia mashine na kwamba viungo muhimu kama vile figo na moyo havifanyi kazi. Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa, kidhahiri huenda Mfalme Abdullah alifariki dunia tangu Jumatano ya wiki jana na kwamba jambo hilo limefichwa ili kuepusha vita vya kung'ang'ania madaraka huko Saudi Arabia. Hii ni katika hali ambayo, Mfalme Abdullah hajaonekana hadharani kwa muda mrefu sasa. Duru za karibu na familia ya al-Saud zinaarifu kuwa, baadhi ya watu wenye ushawishi hawamuungi mkono mrithi wa sasa wa ufalme, Salman bin Abdulaziz. Katika siku za hivi karibuni kumeripotiwa vita vya ung'ang'aniaji madaraka miongoni mwa watu mashuhuri wa familia ya al-Saud nchini humo. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/32187-ripoti,-huenda-mfalme-wa-saudia,-amefariki,-dunia