Viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbulla wametoa onyo kwa magaidi Syria kuwa, harakati hiyo haitotetereka wala kurudi nyuma kutokana na vitisho vya magaidi hao. Sayyid Hashim Safiyyudin, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ameyasema hayo hii leo sambamba na kulaani mashambulizi ya maroketi ya magaidi huko kusini mwa Lebanon na kuongeza kuwa, watendaji wa jinai hiyo ni watu waovu ambao wameajiriwa na vibaraka wa Marekani na waitifaki wao katika eneo hili. Amesisitiza kuwa, ni wadhifa wa serikali ya Lebanon kuwatambua na kuwaadhibu wale wote waliowasaidia magaidi hao kufanya shambulizi hilo. Kwa upande wake Naibu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah Sheikh Nabil Kaouk amesema kuwa, jinai hizo haziwezi kamwe kuifanya harakati hiyo ibadili mwelekeo wake na kwamba Hizbullah haiwezi kutetereka hata chembe. Shambulizi la roketi huko kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon limepelekea mtu mmoja kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, shambulizi hilo limefanyika baada ya Katibu Mkuu wa Harakati hiyo ya Hizbullah Seyyed Hassan Nasrullah kutangaza kuwa, muqawama hauwezi kuangalia kwa macho tu jinsi magaidi wanavyofanya mauaji ya watu huko nchini Syria. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/32223-hizbullah-ya-lebanon-yawaonya-magaidi-wa-syria
HIZBULLAH YA LEBANON YAWAONYA MAGAIDI WA SYRIA.