Iran imelaani vikali uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuwaondolea vikwazo vya silaha magaidi wanaoendesha mapigano dhidi ya serikali ya Syria.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Seyyed Abbas Araqchi amesema hayo leo Jumanne na kuutaja uamuzi huo kuwa wa 'hatari'.
Jana Jumatatu Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya walikutana Brussels Ubelgiji na kuafiki suala la kuondoa vikwazo vya kutumiwa silaha magaidi wanaoipiga vita serikali halali ya Syria. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, uamuzi huo wa EU utapelekea hali ya Syria kuzorota zaidi na kuzuia juhudi za kimataifa za kuusuluhisha kisiasa mgogoro wa nchi hiyo. Araqchi aidha kwa mara nyingine amesisitiza kuhusu msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za amani. Ameongeza kuwa Tehran imezialika nchi 40 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa, utakaojadili njia za kutatua mgogoro wa Syria. Mkutano huo utafanyika kesho tarehe 29 Mei hapa mjini Tehran. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/32221-iran-yalaani-uamuzi-eu-wa-kuwapa-silaha-magaidi-syria