Makundi ya kigaidi nchini Syria yamepokea shehena mpya ya tani 35 za silaha kutoka serikali ya Saudi Arabia. Salim Idriss mmoja kati ya viongozi wa Baraza la Kijeshi la kundi la kigaidi liitwalo 'Jeshi Huru la Syria' kutoka Amman nchini Jordan kwamba, kundi hilo limepokea silaha mpya kutoka Saudi Arabia kwa shabaha ya kupambana na majeshi ya serikali ya Syria.
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, Salim Idriss pia ameitaka serikali ya Marekani iwapatie kuanzia mwezi ujao magaidi hao wa Syria kila wiki tani 700 za silaha na zana za kijeshi. Hivi karibuni Robert Stephen Ford balozi wa zamani wa Marekani nchini Syria alifanya safari katika eneo la mpaka wa Syria na Uturuki na kusambaza shehena za silaha kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa pamoja tokea mwezi Machi 2011 zimekuwa zikiwasaidia magaidi wa Syria ambao wengi wao wanatoka nchi za Kiarabu kwa shabaha ya kufanya mauaji na kuvuruga amani na uthabiti nchini Syria. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/32082-magaidi-wa-syria-wapokea-silaha-kutoka-saudia