Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran
amesema kuwa, kushiriki kwa wingi wananchi wa Iran katika duru ya 11 ya uchaguzi wa rais utakaofanyika Juni 14 mwaka huu ni wajibu ili kukabiliana na njama za maadui. Huku akiashiria sisitizo la Mtume Mtukufu SAW la udharura wa kulinda umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema, Mtume Muhammad SAW aliharamisha kushambulia Waislamu wengine na mali zao. Aidha ameeleza kuwa, Waislamu wanapaswa kutoingia katika mtego wa maadui wa Uislamu kwa kuwa na taasubu za kimadhehebu, hivyo Waislamu wote, Mashia na Masuni wanapaswa kuungana na kukabiliana na njama za adui za kuhujumu Qur'ani Tukufu na fikra za Kiislamu.Aidha sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa kuadhimisha kuzaliwa Bibi Fatwimatu Zahraa (A.S) binti kipenzi wa Mtukufu Mtume SAW na Siku ya Mwanamke pamoja na Siku ya Mwalimu, Ayatullah Imami Kashani amesema, nafasi na thamani ya mwanamke na mwalimu katika Uislamu ni ya juu sana.
Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/31602-kushiriki-wananchi-katika-uchaguzi-kutazima-njama