Mkuu wa Baraza la Kidini la Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran ni mshika bendera wa umoja na mshikamano wa Kiislamu ulimwenguni.
Sheikh Muhammad Yazbek ameongeza kuwa, Iran kwa kuunga mkono kadhia ya
Palestina imeweza kuonyesha kivitendo umoja na mshikamano wa Waislamu na
kusisitiza kuwa jambo lolote linalozungumzwa kinyume na uhakika huo, litakuwa
ni katika mwendelezo wa mikakati na njama chafu za Marekani na waitifaki wake
katika eneo za kuichafua Iran. Sheikh Yazbek ameongeza kuwa, kama madola ya
kibeberu ya Magharibi yataacha uungaji mkono wao kwa makundi ya magaidi nchini
Syria, wananchi wa nchi hiyo wataweza kutatua mgogoro uliopo kwa
njia ya mazungumzo. Mkuu wa Baraza la Kidini la Hizbullah ya Lebanon amesema
kuwa, iwapo serikali ya Rais Bashar al Assad itapinduliwa huko Syria basi jambo
hilo litabadilisha kabisa mustakbali wa Wapalestina na kadhia nzima ya Palestina
ulimwenguni.
Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/31444-iran-ni-mshika-bendera-ya-umoja-wa-kiislamu