Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,
ametoa hukumu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa Katibu wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, huku
akiwaachia huru wafuasi wake 49 waliokuwa wamejumuishwa kwenye kesi
yake. Kwa mujibu wa duru za Tanzania, Sheikh Ponda na wenzake walikuwa
wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la uchochezi. Awali Wakili wa
Utetezi, Juma Nassoro akitoa hoja za majumuisho mbele ya Hakimu Victoria
Nongwa aliiomba Mahakama iwaone washitakiwa hawana kesi ya kujibu, kwa
kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kujenga kesi na kuthibitisha tuhuma
dhidi ya washitakiwa.