Shirika la
Haki za Binadamu
la Human Rights Watch HRW limesema kuwa maafisa wa Myanmar
wameanzisha kampeni ya kuangamiza kizazi cha Waislamu wa Rohingya nchini humo.
Kundi hilo la kutetea haki za binadamu leo limetoa taarifa na kueleza kuwa
wimbi la ghasia na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa Rohingya wa Myanmar
limesababisha kuuliwa mamia ya watu na kuwafanya maelfu ya wengine huko katika
jimbo la Rakhine maghariribi mwa nchi hiyo kuwa wakimbizi mwaka jana.
Likiashiria ushahidi wa makaburi ya umati na hatua ya Waislamu hao kulazimika
kuyahama makazi yao huko Myanmar, Human Rights Watch limeeleza kuwa serikali ya
Myanmar ilishiriki katika kampeni ya kuangamiza kizazi cha Waislamu wa
Rohingya, kampeni ambayo inaendelea hadi leo hii kutokana na serikali hiyo
kuzuia kufikishiwa misaada raia hao na kuwawekea vizuizi mbalimbali raia hao.
Kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/31330-waislamu-wa-myanmar-wanakabiliwa-na-maangamizo