Sheikh Said Othuman
amesema, Mkoa wa Iringa
unahali mbaya kiharakati kwani mpaka sasa kuna Mashia tabiribani wa
tano, pia Mashia hao wa tano mpaka sasa hawana Mwalimu bali wanachumba
tu chakusomea, kwa kweli Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s) bado
hayajafika Mikoani kikamilifu kama baadhi ya watu wanavyofikiria, kwa
kweli Sheikh Hemed Jalala, anasitahiki pongezi kwa Fikra zake za
kufikisha ujumbe wa Ahlul-Bayt (a.s), katika sehemu za Mikoani, kwani
amesaidia sana mpaka sasa napenda kusema hao Wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s)
waliopatikana katika sehemu ya Iringa wamepatikana baada ya msafara wa
Sheikh Hemed Jalala pamoja na jopo lake la Tabligh, lilipofika Iringa na
kufanya Mudhara kwa mara ya kwanza, kwa kweli hali ni mbaya kwa upande
wetu kama Wafuasi wa Ahlul-Buyt (a.s), inatubidi tutambue kuwa bado
tunajukumu kubwa katika kufikisha mafundisho sahihi ya Bwana Mtume
Muhammad (s.a.w.w) katika jamii yetu ya Tanzania.