Katibu Mkuu wa Jumuiya
ya Kimataifa
ya Mwamko wa Kiislamu amesema kuwa, kudai uhuru na kutaka Uislamu ni matakwa ya
wanamapinduzi Waislamu yasiyoweza kutenganishwa. Ali Akbar Wilayati amesema
hayo mjini Tehran katika siku ya kwanza ya kikao cha Kimataifa cha Mualamaa na
Mwamko wa Kiislamu na kuongeza kuwa, kuswaliwa swala za jamaa, Ijumaa na
kustafidi na nara na nembo za kidini katika maandamano ya wanamapinduzi wa
Kiislamu kunaonesha kuwa, matakwa hayo mawili hayatengani. Huku akibainisha
kuwa baada ya kuanza wimbi jipya la mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu
za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, madola ya Magharibi yalianzisha
jitihada kubwa za kupora harakati hiyo, Wilayati amesema Wamagharibi walitaka
kupoteza sura ya Kiislamu ya harakati hiyo ili ionekane kuwa ya kudai uliberali
na demokrasia ya Magharibi. Pia ameshiria kuundwa Jumuiya ya Kimataifa ya
Mwamko wa Kiislamu na kusema kuwa, kutokana na uvumbuzi wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran Septemba 2011 zaidi ya washiriki 700 wakiwemo wanafikra, viongozi,
shakhisia tofauti na wanaharakati wa sekta mbalimbali kutoka nchi tofauti
duniani walikusanyika mjini Tehran ili kujadili masuala tofauti yanayohusu
wimbi la mwamko wa Kiislamu, changamoto na matarajio, na hapo ndipo
Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu ilipoasisiwa. Kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/31514-uhuru-na-uislamu,-mihimili-mikuu-ya-wanamapinduzi