Maulana Sheikh Hemed Jalala,
Mudir wa Hawzat
Al-Imam Swaadiq (a.s), Kigogo Post, Dar es Salaam, akitoa Historia fupi
juu ya Tarekhe ya Kiislaam, Wilayani Kondoa.
Wakina mama wa Kiislaamu wakiwa katika Darasa la Ujue Ushia, lililofanyika Kondoa Mjini, kwa muda wa siku mbili mfululizo.
“Ee Mola (wabariki) na wafuasi wa Mitume
(wote) na wale wenye kuwasadikisha katika mambo ya ghaibu, wakati
wapinzani wao wanapowapinga kwa kuwakadhibisha, hali wao wana hamu ya
(kuwaona) Mitume kwa imani ya kweli, katika kila wakati na zama,
(ambapo) ulitumwa Mtume na ukawasimamishia watu wake dalili ya Maimamu
na uongofu na viongozi wa wacha Mungu, amani iwe juu yao wote.
(Tafadhali) wakumbuke (wote) hao kwa maghfira na radhi (zitokazo kwako).
Ee Mola! (wabariki) na Sahaba wa Muhammad hasa, ambao waliandamana naye
kwa wema, na ambao walipigana kishujaa katika Kumnusuru, wakamsaidia na
kufanya haraka katika kuunga mkono ujumbe wake na kuuitikia mwito wake,
waliomwitikia mara tu alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake,
wakajitenga na wake (zao) na watoto (wao) katika kuthibitisha Utume
wake, na wakanusurika kwaye.
(Wabariki) na wale waliozama katika kumpenda yeye, waliotarajia biashara isiyoweza kuharibika ya mapenzi (yao) kwake. (Wabariki) na wale ambao jamaa zao waliwahama pale waliposhikamana na kishiko (imani) yake, na (wale ambao) akraba (zao) waliwakimbia pale walipokaa chini ya kivuli cha akraba zake. Basi usisahau, ee Mola! Yale waliyoyaacha kwa ajili yako katika njia yako. Wape radhi zako kwa kuwakusanya viumbe (vyako katika dini yako), na kwa kuwa walinganiaji wako pamoja na Mtume wako, (waliolingania watu) kwako. Uwalipe kwa kuyahama Majumba ya watu wao kwa ajili yako, na kwa kutoka kwenye maisha ya ufanisi na kuingia katika yale ya dhiki, na kwa mateso mengi yaliyowapata katika kuitunza dini yako.
Ee Mola! Uwafikishie bora ya malipo yako wale waliowaandamana wao kwa wema ambao wakisema: “Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani. Ambao wameamua kufuata njia yao iliyowazi na kuelekea mwelekeo wao, wakafuata nyayo zao, ambao shaka haikuwatoa katika dini yao wala haikuwababaisha katika kuzifuata njia zao na kuongoka kwa uongozi wao, huku wakiwasaidia na kuwatia nguvu, waliofuata dini yao na kuongoka kwa kiongozi wao, wakaafikiana nao bila ya kuwatuhumu katika yale waliyowafikishia.
Ee Mola! Warehemu na waandamizi (wa Maswahaba), kutoka siku yetu hii mpaka siku ya malipo. (Uwarehemu) na wake zao, vizazi vyao, na wale waliokutii wewe miongoni mwao, kwa rehema ambazo kwazo utawakinga na kukuasi wewe, utawakunjulia bustani za Pepo yako, utawakinga kwazo na vitimbi vya shetani na kuwasaidia katika mema waliyokuombea msaada, utawakinga na vituko vya usiku na mchana isipokuwa kituko kiletacho kheri, uwapelekee kwazo kuwa na imani ya kutarajia mema kwako, kuwa na tama ya yaliyoko kwako, na kuacha kutuhumu yaliyomo mikononi mwa waja (wako), ili uwarejeze katika kujipendekeza kwako na kuogopa, (na ili) uwafanye weupe mgongo ufanisi wa dunia (hii) na kuwapendekezea kuiendea mbio Akhera na kujitayarisha kwa yaliyoko baada ya mauti, (ili) uwafanyie jepesi kila zito litakalowazunguka siku ya roho kutoka miilini mwao, uwaa’fu na makatazo yote yale ambayo huletwa na mitihani, (uwaa’fu) na mateso ya Moto na kubaki humo milele, na (ili) uwapeleke kwenye amani ya makazi ya wacha Mungu.”

Wakazi wa Kondoa wakiwa katika Muhadhara wa Ujue Ushia, uliofanyika siku ya J.mosi.