“Hakika Mwenyezi Mungu amejifaharisha kwenu,
hivyo akawasamehe nyinyi wote kwa ujumla na akamsamehe Ali mahsusi, na
hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, si mwenye kuogopwa kwa
ajili ya watu wangu na ni mwenye kupendwa kwa sababu ya
kizazi changu. Huyu hapa Jibril ananipa habari kuwa: Mwema wa kweli ni
yule atakayempenda Ali wakati wa uhai wangu na baada ya kifo changu.”
Taz: Asnal-Matwalib cha Shamsud-Din Al-Jazriyyu, 70.