"Ewe Mwenyezi Mungu, hakika wewe
unafahamu kuwa yale yaliyotoka kwetu hayakuwa kwa ajili ya kugombania
utawala wala kupata chochote kati ya mabaki ya kinachosagika. Lakini
yalitoka kwa ajili ya kuhami mafunzo ya dini yako na kudhihirisha wema
katika nchi yako, ili wasalimike wale waliodhulumiwa miongoni mwa waja
wako na zifanyiwe kazi hukumu zako zilizoachwa."