SHEREHE YA KUZALIWA MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W), ILIYOFANYIKA JAMIATUL MUSTAFA UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM.

Sayyed Shaheed,
 akitoa salamu zake katika sherehe ya Maulid, ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), iliyofanyika Jamiatul Mustafa, Upanga, jijini Dar es Salaam.
 Kulia Balozi wa Jamuhuri ya Kiislam ya Iran, 
akiwa karibu na Imam (katikati) wa Msikiti wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), Koja, uliyopo Posta jijini Dar es Salaam, wakiwa katika Sherehe ya Maulid ya Mtume (s.a.w.w), iliyofanyika Jamiatul Mustafa Upanga, jijini Dar es Salaam.
 Kusherekea Mazazi ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kuzitukuza sifa zake ambazo zimesifiwa na Mwenyezi Mungu. Nabii Issa (a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu amteremshie meza ya chakula, na siku hiyo ya kuteremshwa meza ya chakula aliitaja kuwa ni siku ya Sikukuu: "Ee Mwenyezi Mungu Mola wetu! tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu na kiwe ishara itokayo kwako, na turuzuku, kwani wewe ni mbora wa mbora wa wanaoruzuku." 5:114

Swali: Je, thamani ya kuwepo Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni ndogo kuliko meza ya chakula kilichotoka mbinguni ambacho Nabii Issa (a.s) ametangaza siku ya kuteremshwa chakula hicho kuwa ni Sikukuu? Ikiwa kufanywa siku hiyo Sikukuu ni kwa sababu ya chakula ilikuwa ni ishara ya Mwenyezi Mungu, Basi Je, Bwana Mtume (s.a.w.w) si ishara kubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia rehema Mtume, na Malaika wake wanamteremshia rehema Mtume, enyi mlioamini! Muombeeni rehema (Mtume) na muombeeni amani" 33:56.
Iliposhuka Aya hii, Maswahaba waliuliza: Watamuombeaje rehema? Bwana Mtume (s.a.w.w) akawafundisha, semeni: "Allahumma Swalli A'laa Muhammad wa Aali Muhammad. Hili ni muhimu sana kulielewa, kwa sababu, wako watu wengine wanapomuombea rehema Mtume husema: Swallallahu Alayhi Wasallama. Hii ni kosa, kwa sababu Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakufundisha hivyo. Bali amesisitiza kwa kusema: "Msiniombee rehema kwa kunikata, mkisema: Allahuma Swalli A'laa Muhammad wa Aali Muhammad.

Taz:
Sublus Salaami J.1 Uk. 326