Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,
alikuwa mgeni
rasimi wa Sherehe ya Maulid ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika
Sherehe hiyo amezungumzia juu ya swala zima la Amani ya inchi ya
Tanzania, amesema katika inchi ya Tanzania wanaishi watu mbalimbali
wapo watu wenye dini na watu wasio na dini, chamsingi ni kuvumiliana
hili kila mmoja wetu haweze kuishi, mwisho kamalizia kwa kuwataka
Viongozi wa dini kuamasisha amani pindi wanapokuwa katika majukwaa yao.
Ummah wa Kiislam umefurika katika ukumbi wa
Daimond Jubilee, kwa ajili ya kushereheka juu ya mazazi ya Bwana Mtume
Muhammad (s.a.w.w), Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: "Hakika Mwenyezi
Mungu na Malaika wake humsalia Mtume, enyi mlioamini! msalieni (Mtume)
na muombeeni amani." 33:56
Maulana Sheikh Hemed Jalala,
Mudir wa Hawzat
Al-Imam Swaadiq (a.s), Kigogo Post, Dar es Salaam,(katikati), akiwa
katika hali ya furaha baada ya kuona Ummah wa Kiislam ulivyofurika
katika ukumbi wa Daimond Jubilee,jijijni Dar es Salaam.
Sayyid Shaheed,
(katikati) kiongozi wa chuo
cha Jamiatul Mustafa University, kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam,
akiwa katika Sherehe ya Maulid ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w),
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waumini wa Madhihabu mbalimbali za Kiislam,
wakiwa katika Sherehe ya Maulid ya kipenzi cha Mwenyezi Mungu, Mtukufu
Mtume Muhammad (s.a.w.w), yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,
jijini Dar es Salaam.
Tarehe: 17-02-213
Tarehe: 17-02-213