Bismillahir Rahmanir Rahim.
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alitumia muda wake mwingi zaidi nyumbani huku hakijihusisha na kazi ya kuzikusanya Aya za Qur'an, na kuzipanga katika kufuata utaratibu wa miaka na matukio. Alikuwa kwa hiyo anadhihirisha kwamba kazi yake ilikuwa ni kutumikia Uislamu licha ya mazingira yasiyofungamana nayo. Mara nyingi alidondoa, mbele ya marafiki zake, zile Hadithi za Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwamba watu wa nyumba yake na Qur'an ndio vilikuwa "mirathi" yake kwa Umma wa Waislamu, na kwamba vyote hivyo havitenganishiki kimoja kutoka kingine.
Hakuna hata mmoja kati ya Maswahaba aliyekuwa na ujuzi bora zaidi kuliko Imam Ali bin Abi Talib (a.s) wa kuzikusanya Aya za Qur'an. Alikuwa mmoja kati ya Maswahaba wachache wa Bwana Mtume (s.a.w.w) walioijua Qur'an kwa moyo.
Kwa bahati mbaya, Umar Ibn Al-Khattab alitumia miaka kumi na nne akijaribu kuhifadhi Sura ya pili ya Qur'an (Al-Baqarah), lakini hakuweza.
Kukusanya Aya zote za Qur'an zilizotawanyika, katika mpangilio ule ule zilishuka, ilikuwa ni kazi ambayo ingeweza kufanywa na mtu mahsusi aliyedarisishwa na Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) wenyewe. Mtu kama huyo alikuwa ni Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Alikaa muda mwingi naye kuliko mtu mwingine yeyote yule. Alikuwa, kwa maneno halisi, amekuwa na Qur'an. Yeye mwenyewe alisema kuwa haikuwepo Aya yeyote katika Qur'an, juu yake ambayo alikuwa hajui ni lini ilishuka, wapi ilishushwa, na kwa nini ilishushwa. Alikuwa anajua wakati, mahali na tukio la kushuka kwa kila Aya ya Qur'an.
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) aliimaliza kazi hiyo aliyojipa mwenyewe. Lakini bahati mbaya kwa Uislamu, kundi lililokuwa Madarakani, kwa kufuata sera zao, halikutaka kuitambua kazi yake. Hakuna kitu ambacho kilikuwa hakitakwi na kundi hilo kuliko kutambua utumishi wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) kwa Uislamu. Halikuwa kwa hiyo, "limeukabili" mkusanyiko wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) wa Aya za Qur'an.
Katika siku zilizofuatia mara tu baada ya kifo cha Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), watu wengi walikuja kumuona Imam Ali bin Abi Talib (a.s), na baadhi yao walimshauri kutwaa kwa nguvu kilichokuwa chake kihalali.
Miongoni mwa watu hawa walikuwapo marafiki wa kweli wachache, na pia walikuwepo wafuata maslahi binafsi wengi wasiokuwa na maadili. Wote walimuahidi kumuunga mkono. Hawa wa kundi la mwisho, kwa kweli, waliahidi uumungaji mkono wao kwa sababu zilizofichika. Walitarajia kuchochea vita katika Uislamu na kunufaika katika mashindano ya kikatili ya Waislamu.
Mara tu baada ya kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w), ami yake, Abbas Ibn Abdul Muttalib, alimwendea Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na kusema: "Nyoosha mkono wako, nami nitakupa kiapo changu cha utii.
Kitendo changu hiki cha kuonyesha hisia kitakuwa na athari kubwa ya kisaikolojia juu ya Waislamu. Watasema kwamba ami yake Mtume ametoa kiapo chake cha utii kwa Ali; nasi pia, kwa hiyo, tumpe yeye kiapo chetu."
Abbas, kwa kweli, alikuwa mmoja wa hao marafiki wa kweli wachache. Katika kundi jingine la "watakia heri" wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alikuwa ni Abu Sufyan, kiongozi wa Bani Umayyah, adui wa milele wa Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), alama ya upinzani na chuki kwa Uislamu. Katika matukio yaliyofuatia kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w), aliona fursa yake ya kuuangamiza Uislamu, na aliitumia. Alikuja kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na akasema: "Inafedhehesha mno kuona watu wa koo duni kabisa za Quraishi zikipora haki yako, na kuikamata serikali ambayo ni yako.
Unachotakiwa kufanya ili kuichukua kutoka kwao, ni kunipa mimi ishara, nami nitaijaza mitaa ya Madina kwa Askari wa chini na wa farasi, waliotayari kufa kwa amri yako."
Binadamu gani angeweza kuikataa ahadi hii? Na alikuwa na nini cha kupoteza sasa hata hivyo? Ambacho angepoteza, alikwisha kipoteza. Lakini basi ni nani katika umma wa Waislamu aliyeupenda Uislamu kama yeye alivyoupenda? Yeye kamwe hakuruhusu vishawishi au uchokozi kumfanya yeye afanye kitu chochote ambacho kingezuia maslahi makubwa zaidi ya Uislamu na Waislamu. Uislamu ulikuwa bado ni mafanikio hafifu yenye uwezekano kabisa wa kuharibiwa na kupotoshwa na nguvu ndani na nje ya Madina lakini Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ulikuwa na mlinzi ambaye hakuruhusu hilo litokee.
Kama Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alikuwa ndiye "Hakimu bora katika Uislamu," alikuwa pia ni hakimu mzuri wa watu. Jibu lake kwa Abu Sufyan, liliundwa kama swali, lilikuwa bainishi. "Tangu lini umekuwa mtakia heri wa Uislamu?" aliuliza Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Lilikuwa ni swali la kiufasaha tu, na kwalo tu aliibeua ahadi ya Abu Sufyan kwa dharau ambayo ilistahili, na akamtolea sauti ya mfyonzo.
Kwa jibu hili, Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alidhihirisha kwa mara nyingine tena kwamba yeye na yeye peke yake ndiye aliyekuwa mlezi wa kweli hasa wa Uislamu. Katika wakati huu wa kuamua hatima yake, aliyaacha maslahi na matamanio yake binafsi lakini aliuokoa Uislamu kutokana na kuangamia.
Ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya Uislamu mchanga. Maasi dhidi ya Serikali ya Abubakr bin Abi Quhafa yalikuwa yakitokea ghafla kote nchini. Kama Imam Ali bin Abi Talib (a.s) angezikubali ahadi za ami yake, Abbas Ibn Abdul Muttalib, na za Abu Sufyan, angeweza kufanikiwa kuikamata Serikali ya Madina. Lakini mafanikio yake yangekuja kwa gharama tu, kwa Uislamu, ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hapo Madina ambapo palikuwa ndio kiini cha dola ya Uislamu na jamii. Vita ndani ya Madina kwa hali ya mambo yalivyo ingeweza kusimamisha ghafla kazi ya Uislamu.
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) aliushinda mtihani huu kama alivyoshinda mingine mingi maishani mwake. Hakushawishika na matamanio.