"Kwa kadiri gani niwatendee kwa upole kama atendewavyo ndama wa ngamia aliyeraruka nundu yake kwa ndani, na nguo iliyochoka, kila ishonwapo upande mmoja wararuka upande wa pili, na wanapokupitieni askari wa Sham, kila mmoja wenu huufunga mlango wake, na hutokomea utokomeaji wa guruguru shimoni mwake, na fisi ndani ya tundu lake.
Wallah dhalili ni yule mliyemnusuru! Na mwenye kutupa mshale kwa msaada wenu ni sawa na atupae mshale uliovunjika pande zote mbili. Ninyi mnakuwa wengi kwenye kumbi za nyumba, na mnakuwa wachache chini ya bendera. Mimi najua kinachoweza kuwarekebisha, na kunyooshaa kupindama kwenu, lakini mimi Wallah sitowarekebisha kwa kujiharibu binafsi. Mungu azidhalilishe nyuso zenu, na aangamize hadhi zenu, hamuujui ukweli kama muijuavyo batili, wala hamuibatilishi batili kama mubatilishavyo ukweli." (Imam Ali bin Abi Talib (a.s), katika Nahju'l - Balaghah)