"Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio
pamoja naye ni (wenye nyoyo) imara mbele ya makafiri na wenye
kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama na wakisujudu wakitafuta
fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi yake. Alama zao ni katika nyuso zao
kwa athari ya kusujudu, huo ndio mfano wao katikaTaurati, na mfano wao
katika Injili: Kama mmea uliotoa matawi yake, kisha yakautia nguvu,
ukawa mnene ukasimama sawa sawa juu ya shina lake ukawafurahisha walio
upanda, ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu
amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na malipo
makubwa."
Qur'an: 48:29
Qur'an: 48:29