Sayyed Haidarusi,
amesema Bwana Mtume Muhammad
(s.a.w.w), alikuwa Mkubwa katika kila nyanja wakati wa huai wake, kwa
hiyo Waislam hawanabudi nao kuwa wakubwa katika mambo yao, amesema hayo
Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post, jijini Dar es Salaam.
Waumini wa Madhihabu ya Ahlul - Baty (a.s),
wakiwa katika maombolezo ya kifo cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w),
yaliofanyika Masjid Ghadiir Khum, Kigogo Post jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Shia Ithna Ashariya Tanzania,
Sheikh Abdallah Seif, akiwa na Vijana katika Maombolezo ya Kifo cha
Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), yaliyofanyika Kigogo post, jijini Dar
es Salaam, Tanzania.
Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) amefariki tarehe 28 Swafar siku ya Jumatatu mwaka wa kumi Hijria. Familiya ya Bwana Mtume ikakusanyika kwa ajiri ya mipango ya maziko. Umar bin Khattab alivyoona hivyi, alichukua upanga akawa anazunguka huku na kule katika eneo la Msikiti na nyumba ya Bwana Mtume. Umar bin Khattab kwa sauti yake ya juu akawa anaonya: "Wanafiki wanasema Mtume amefariki, na hakika Mtume hakufa, atakaesema Mtume amekufa nitakata shingo yake." Mpaka alipofika Abubakar bin Abu Quhafa akitokea kijijini Sunhi kwa mke wake, akaingia ndani alipolazwa Bwana Mtume (s.a.w.w). Alipotoka akasoma Aya: Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na Mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu? Na atakaerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru." Qur'an: 3:144.
Umar bin Khattab akasema: "Wallahi, kana kwamba watu hawajui kuwa Aya hii ilishuka kwa Mtume." Kisha Abubakar bin Abu Quhafa na Umar bin Khattab wakaondoka kuelekea katika ukumbi wa Bani Saaidah kwa ajili ya Uchaguzi.
Taz: Tarekhut Tabari J. 3 Uk. 67 - 69
Tarekh Ibn Athir J. 2 Uk. 219
Kumbuka, Umar bin Khattab anasema: "Wanafiki wanasema Mtume amekufa." Je, ni wakina nani wanafiki? Nyumbani kwa Bwana Mtume walikuwapo: Ali bin Abi Talib, Fatma bint Muhammad, Abbas bin Abdil Muttalib, Alfadhul bin Abbas, Qutham bin Abbas na Usama bin Zayd. (ilipotangazwa kuwa Mtume amefariki, Usama pamoja na kundi lake la jeshi walirejea mjini) Hawa ndio walikuwamo nyumbani pamoja na mwili wa Bwana Mtume, na ndio waliotangaza kuwa Bwana Mtume amefariki. kwa fikra za Umar bin Khattab, hawa ni wanafiki, na ndio wanaositahiki kukata shingo zao!!!
Abubakar bin Abu Quhafa na Umar bin Khattab hawakuhudhuria katika osho wala maziko ya Bwana Mtume, wao walikuwa katika ukumbi wa Bani Saaidah wakichaguana!!!
Taz: Kanzul Ummal, Kitabul khilafa maal-imaara khilafatu Abibakar
Almuswannaf, cha Ibn Shayba, babul Maghaz khilafatu Abibakar
Pia Mkewe Aisha hakuhudhuria osho wala maziko ya Bwana Mtume, alipotea nyumbani kwa Bwana Mtume siku mbili, mwenyewe Aisha anasimulia: "Wallahi hatukuelewa maziko ya Mtume mpaka tuliposikia kelele za majembe usiku wa jumanne (wakati wakichimba kaburi):
Taz: Assunanul Kubra, J. 3 Uk. 574
Tarekhut Tabari J. 3 Uk. 81
Al-muntadham J.2 Uk. 482
Kifo cha Bwana Mtume kinamashaka, Je, amekufa kifo cha kawaida au ameuliwa kwa Sumu? Anasema mkewe Aisha kuwa: Tulimwenywesha dawa Mtume wakati wa maradhi yake, na Mtume akiwazuia: "Msininyweshwe."
Taz: Tarekhut Tabari J.3 Uk. 62
Fat-hul Baary J. 10 Uk. 175
Waandishi wa Kiislam wanasema kuwa: Waliohusika kumnywesha dawa hiyo kwa nguvu ni Aisha na Hafsa (wake zake Mtume) na kwamba dawa hiyo ni Sumu!!
Taz: Assiratun Nabawiyya, ya Najahu Attaai J. 2 Uk. 379
Alburhan fyitafsiril Qur'an J. 2 Uk. 117
Tafsirus Saafy J. 1 Uk. 389 - 390
Tafsirul A'yyaashy J. 1 Uk. 224
Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) alioshwa na kuswaliwa, kuzikwa na: Ali bin Abi Talib, Abbas bin Abdul Muttalib, Qutham bin Abbas, Alfadhul bin Abbas na Usama bin Zayd. Bwana Mtume Muhammad (s.aw.w) amezaliwa siku ya Jumatatu, amepewa Utume siku ya Jumatatu, amehama Makka kwenda Madina siku ya Jumatatu, amefika Madina siku ya Jumatatu, na amefariki siku ya Jumatatu.
Taz: Almuntadham J.2 Uk.477
Tarekhut Tabari J.3 Uk. 80
Wanawake nao hawakuwa nyuma katika kumuenzi Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika matembezi yaliyofanyika Kigogo post, jijini Dar es Salaam.