SEMINA ILIYOJUMUISHA MASHIA KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI.

Mwenyekiti wa Tanzania Ithna Ashariya Community,
amesema katika Semina iliyofanyika Makao Makuu Tanzania Ithna Ashariya Community, Kigogo post, jijini Dar es Salaam, kuwa lengo letu ni kujenga kuleta mshikamano kuwa wa moja kuendeleza kutangaza fikra na maelezo msimamo elimu fikra za Ahlul - Bayt (a.s), kwa nini tuwe mbali mbali katika kuyapigania Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), amemalizia kwa kusema huu ni wakati wa mabadiliko kwa wafusi wa Ahlul-Bayt (a.s), na kufanya kazi kwa umoja na mshikamano hili kuleta umoja na usawa katika taasisi yatu ya Tanzania Ithna Ashariya Community iliyopo Kigogo post, jijini Dar es Salaam.
 Waumini wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s) kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika Semina iliyofanyika Makao Makuu ya Mashia wa Tanzania, Kigogo post, jijini Dar es Salaam, kwa muda wa siku mbili J.mosi na J.pili.
  "Na shikamaneni na kamba ya Mwenyeezi Mungu nyote wala msifarakane. Na kumbukeni neema ya Mwenyeezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema yake mkawa ndugu, na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto naye akakuokoeni nalo. Hivyo ndivyo Mwenyeezi Mungu anavyokubainishieni dalili zake ili mpate kuongoka."
SUURA AALI IMRAAN. Aya ya 103.