WAISLAMU WA ARUSHA WAFANYA AROBAINI YA IMAM HUSSEIN (A.S), MJUKUU WA MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).

Sayyed Haidarusi 
kutoka lamu Kenya, alikuwa mgeni rasimi na mzungumzaji katika Arobaini ya Imam Hussein (a.s) iliyofanyika Mkoani Arusha.
 Waislamu wa Madhihabu mbalimbali ya Kiislamu na Wanaharakati wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika Arobaini ya Imam Hussein (a.s) Mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliyejitoa Muhanga siku ya Ashura, maisha yake na familia yake na Masahaba zake kwa ajili ya Haki na Ubinadamu uliokuwa umekanyagwa na Mtawala dhalimu Yazid Ibn Muawiyyah. Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na kizazi chake.
Sheikh Abdurazaki Musuya 
akizungumzia masaibu ya Imam Hussein (a.s) siku ya Arobaini yaliyofanyika Arusha.