Bismillahir Rahmanir Rahim.
Mwenyezi Mungu anasema: "Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu, ndani yake zimo Aya zilizo wazi wazi nazo ndizo msingi wa Kitabu (hiki) na nyingine ni zenye kufichikana. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu, hufuata yaliyofichikana katika hayo kwa ajili ya kutaka upotovu na kutaka kutafsiri (watakavyo). Na hakuna ajuaye tafsiri yake ila Mwenyezi Mungu na wale waliozama katika elimu tu. Husema: Tumeyaamini, yote yanatoka kwa Mola wetu. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili. Qur'an: 3:7
Iliposemwa: "Na wale waliozama katika elimu" ni Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s).
Taz: Tafsirus Safii J.1 Uk. 318
Al bur'han fyi tafsiril Qur'an J.1 Uk. 271
Majmaul Bayani J.1 Uk 701
Imepokewa Hadith kutoka kwa Abdur Rahman bin Bashir, amesema: Tulikuwa tumekaa mbele ya Mtume (s.a.w.w) akasema: Bila shaka atakufafanulieni mtu katika kuifasiri Qur'an kama nilivyokufafanulieni katika kushuka kwake. Abubakar bin Abu Quhafa akasema: Mimi ndiye? Mtume Muhammad (s.a.w.w) akasema: Hapana. Umar bin Khattab akasema: Mimi ndiye? Mtume Muhammad (s.a.w.w) akasema: Hapana. Lakini mshona viatu, na Ali bin Talib (a.s) alikuwa anashona viatu vya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Kwa hiyo kama ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni mfafanuzi wa Qur'an wakati ikishuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama yalivyotajwa haya katika Aya 105 An Nisaa kuwa: "Hakika tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kama alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu" Basi Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na yeye ni mfafanuzi wa Qur'an katika kuifasiri kisawa sawa baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Taz: Usudul ghaba J.3 Uk. 282
Khasaisun Nasai Uk. 40
Albidayatu Wannihaya J.7 Uk. 398
Mustadrakus Sahihayn J.3 Uk. 122