Bismillahir Rahmanir Rahim.
Mwenyezi Mungu (s.w) anasema: "Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliyoko Makka, ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, ambaye anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia maovu, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini yeye na kumtukuza na kumsaidia na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu. Qur'an: 7:157
Tamko la asili tulilolifasiri kwa "Nabii aliyoko Makka" ni "An-Nabiyyal Ummiyya" ambalo maana yake ni:
1- Nabii ambaye hajui kuandika wala kusoma.
2- Nabii wa Ummah.
3- Nabii aliyezaliwa na mama yake.
(1) Nabii aliyoko Makka, Na hii ni riwaya imepokewa na Imam Muhammad bin Ali Albaaqir (a.s). Na ni riwaya ya sawa
MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ANAJUA KUSOMA.
Utaratibu wa Aya zifuatazo kwa uteremsho wake, unatoa msimamo thabiti kuwa Bwana Mtume (s.a.w.w) alijua kuisoma Qur'an:
. "Tutakusomesha wala hutasahau." Qur'an: 87:6
. "Usiutikise ulimi wako kwa kuufanyia haraka kwa kuisoma (Qur'an)" Qur'an: 75:16
. "Wala usifanye haraka kwa Qur'an kabla haujamalizika kukufikia Wahyi wake, na (uombe) useme: "Mola wangu! Nizidishie elimu." Qur'an: 20:114
Taz: Majmaul Bayan J.2 Uk. 487
Na iliposemwa: "Wale waliomwamini yeye na kumtukuza na kumsaidia na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu."
Maneno yaliyotumika katika Aya hii:
1- Waliomwamini.
2- Wakamtukuza.
3- Wakamsaidia.
4- Wakaifuata nuru.
Wajibu wa kutekelezwa Maf-huum ya maneno haya yanaanzia pale yalipoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na baada yake kwa zama zote.
Ni wajibu kwa kila Muislam katika zama zote, kumwamini Mtume (s.a.w.w) na kumtukuza na kumsaidia pamoja na kuifuata nuru (Qur'an) aliyoteremshiwa.
Kwa hiyo kuwa kusanya watu kwa ajili ya kusherekea Mazazi ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kuzitukuza sifa zake ambazo zimesifiwa na Mwenyezi Mungu. Nabii Issa (a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu amteremshie meza ya chakula, na siku hiyo ya kuteremshwa meza ya chakula aliitaja kuwa ni siku ya Sikukuu: "Ee Mwenyezi Mungu Mola wetu! tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu na kiwe ishara itokayo kwako, na turuzuku, kwani wewe ni mbora wa mbora wa wanaoruzuku." 5:114
Swali: Je, thamani ya kuwepo Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni ndogo kuliko meza ya chakula kilichotoka mbinguni ambacho Nabii Issa (a.s) ametangaza siku ya kuteremshwa chakula hicho kuwa ni Sikukuu? Ikiwa kufanywa siku hiyo Sikukuu ni kwa sababu ya chakula ilikuwa ni ishara ya Mwenyezi Mungu, Basi Je, Bwana Mtume (s.a.w.w) si ishara kubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu?
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia rehema Mtume, na Malaika wake wanamteremshia rehema Mtume, enyi mlioamini! Muombeeni rehema (Mtume) na muombeeni amani" 33:56.
Iliposhuka Aya hii, Maswahaba waliuliza: Watamuombeaje rehema? Bwana Mtume (s.a.w.w) akawafundisha, semeni: "Allahumma Swalli A'laa Muhammad wa Aali Muhammad. Hili ni muhimu sana kulielewa, kwa sababu, wako watu wengine wanapomuombea rehema Mtume husema: Swallallahu Alayhi Wasallama. Hii ni kosa, kwa sababu Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakufundisha hivyo. Bali amesisitiza kwa kusema: "Msiniombee rehema kwa kunikata, mkisema: Allahuma Swalli A'laa Muhammad wa Aali Muhammad.
Taz:
Sublus Salaami J.1 Uk. 326
Yanabiiul Mawadda J. 1 Uk. 6