MAOMBOLEZO YA KIFO CHA IMAM HUSSEIN (A.S), MJUKUU WA MTUME (S.A.W.W), YAMEFANYIKA BILAL, TEMEKE, JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA.

Maombolezo ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s), yamefanyika Bilal Temeke, Jijini Dar es Salaam.
  Sheikh Ghawth Salmu Nyambwa, 
Muhadhir wa Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustaph, kilichopo Upanga, Jijini Dar es Salaam, amewataka watu wote duniani wamuenzi Imam Hussein (a.s), kwa kuwa Imam Hussein (a.s) hakujitoa Muhanga yeye na familia yake kwa ajili ya Ummah wa Kiislam tu, bali alijitoa muhanga kwa ajili ya manufaa ya Ummah wote duniani.
 "Naseme kwamba, hakika mimi nakupigeni  ninyi nanyi mwanipiga mimi, lakini Wanawake hawa hawana kosa lolote, basi hebu wazuiyeni watu wenu hawa waovu na wajinga, wasinivunjie heshima yangu muda wote nitapokuwa ni mzima." Maneno ya Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), akimwambia Shimri,
 Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.
Maulana Sheikh Hemed Jalala,
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), iliyopo Kigogo post, jijini Dar es Salaam,akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza maombolezo ya Kifo cha Imam Hussein (a.s),
yalifanyika Bilal,Temeke, jijini Dar es Salaam.
Maulana Sheikh Hemed Jalala, 
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), akiswalisha Swala ya Adhuhur, baada ya kumaliza kusoma Majris ya Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye alijitoa Muhanga katika Ardhi ya Karbala kwa ajili ya kupinga dhuluma zidi ya Wanadamu.