Upande wa kulia Maulana Sheikh Hemed Jalala, Mudir wa
Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), Kushoto Balozi Jamuhuri ya Kiislamu ya
Irani, wakiwa katika matembezi ya Ashura, yaliyofanyika katika barabara
ya Kigogo, Jijini Dar es Salaam.
Wakinamama wakiwa katika matembezi ya Ashura, yaliyofanyika Kitaifa Kigogo post,
Jijini Dar es Salaam.
Hapana shaka kwamba Bwana Mtume (s.a.w.w)
alihuzunika huzuni nyingi kwa ajili ya kufiwa na Ami yake Abu Talib na
Bibi Khadija Ummul-Muuminina (a.s), kwani wawili hawa walifariki ndani
ya Mwaka mmoja, na Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) akauit
a mwaka huo kuwa ni mwaka wa "huzuni".
Kipindi hiki cha Msiba huu mkubwa, Bwana Mtume (s.a.w.w) alipunguza kutoka, ikawa muda mrefu hukaa nyumbani, na ikawa Maquraishi wanapomhujumu huomboleza kwa kusema:-
"Ewe Ammi yangu imekuwa mapema mno kukukosa."
Taz: Siratul-Halabiya Uk. 462 Juz.1.

Vijana wa Kiislam wamejitokeza kwa wingi
katika barabara ya Kigogo, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuenzi
Imam Hussein (a.s),kutokana na kifo kilichomkumba katika Ardhi ya
Karbala, na jeshi la Yazid ibn Muawiyyah, Laana ya Mwenyezi Mungu iwe
juu yake na wafuasi wake.