Bismillahir Rahmanir Rahim.
Imepokewa kutoka kwa Mama Ummu Salama (mkwewe Mtume) anasema:
"Nilimuona Mtume (s.a.w.w) akikipangusa kichwa cha Imam Hussein na huku akilia, nikamuuliza Unalilia nini? Akasema: "Hivi sasa amenijulisha Malaika Jibril kuwa: Mtoto wangu huyu atauliwa katika Ardhi iitwayo "Karbala" kisha akanipa gao la udongo na akasema: "Huu udongo ndipo mahala atakapouliwa, utunze, siku yoyote utakapogeuka kuwa mwekundu basi ujue ya kwamba amekwisha uliwa."
Ilipofika mwaka wa sitini na moja Hijiria, siku ya Ijumaa (wengine wamesema Jumamosi) Mwezi kumi Muharramu, Imam Hussein bin Ali akauliwa na Jeshi la Yazid bin Muawiyyah. Siku aliyouliwa Imam Hussein mbingu zilimlilia.
Taz: Tafsirul Qurtubi J.16 Uk. 141
Addurrul Manthur J. 5 Uk. 749
Tafsirus Saafi J. 4 Uk. 407
Fat'hulbayani fyi Maqasidil Qur'an J. 12 Uk. 401
Alburhan fytafsiril Qur'an J.4 Uk. 161