HALI YA KISIASA KIPINDI CHA WAKATI WA IMAM RIDHA (A.S).


Kama Waqidi anavyosema: "Imam (a.s) aliwekwa kwa muda mfupi gerezani, muda mwingi Harun Rashid alimuacha Imam Ridha (a.s) peke yake. Hii ni kwasababu kuuliwa kishahidi kwa Imam Musa Kadhim (a.s) kuliwageuza watu wengi dhidi ya Harun Rashid. Kwa hiyo, aliacha mambo yatulie kabla ya kuanza kusababisha madhara yeyote kwa Imam Ridha (a.s).

Pili, Harun Rashid aliofia kuhusu hali ya baadae ya ufalme wake. Aliona matatizo ya kiubuka. Mtoto mkubwa wa Harun Rashid alikuwa ni Muhammad, ambaye alikuwa mashuhuri zaidi kwa jina la Amin. Mama yake Amin alikuwa ni Zubaida, mjukuu wa Mansur Dawanaki. Kwa hiyo, Amin alikuwa ni Bani Abbas kwa mama yake na kwa upande wa baba yake pia alikuwa na madai mazuri kwenye ufalme kuliko mtoto yeyote wa Harun Rashid. Lakini Amin alikuwa sio mtawala mzuri. Alikuwa mpenda anasa ambaye alitumia muda mwingi katika kunywa Pombe na Wanawake kuliko kufikiri kuhusu namna ya kuendesha Serikali yake.

Mtoto wa pili wa Harun Rashid alkuwa ni, Abdulla, mashuhuri kwa jina la Mamun, huyu alikuwa bora zaidi kuliko Amin katika kila njia. Alikuwa makini, mwenye akili na mtawala mzuri. Lakini mama yake alikuwa kijakazi (mtumwa) kutoka Persia (Iran). Hivyo ni wazi asingekubaliwa kama mrithi wa Harun Rashid na ukoo wa Abbas.

Tatizo kubwa la Harun Rashid lilikuwa: Amin alikuwa hafai kuwa Khalifa ajaye lakini hawezi kuachwa kabisa. Mamun alikuwa anafaa kuwa Khalifa lakini hawezi kupewa kila kitu kwasababu Warabu kwa ujumla na hususani Bani Abbas hawatamkubali kama mtawala wao, kwa vile mama yake ni kijakazi.

Basi, akiwa anawajua watoto wake, Harun Rashid alitarajia kwamba watapigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya mamlaka na utawala.

Hatimaye Harun Rashid alikuja na suluhisho ambalo alifikiri litaokoa himaya yake. (Punde hivi tutaona jinsi Harun Rashid alivyokosea). Aliamua kuigawa himaya katika sehemu tatu, kila sehemu ikiongozwa na mtawala tofauti. Alimpa Amin Iraq na Syria mpaka kwenye mipaka ya Magharibi sehemu ya himaya yake. Alimpa Mamun Ardhi yote kuanzia Hamadan Makka mipaka ya mashariki ya himaya yake. Alimpa mtoto wake Al-Kassim Ghuba ya Arabia na bandari ya bahari. Wakati wa kifo cha Harun Rashid, Amin atakuwa Khalifa lakin Mamun na Al-Kassim wataendea kuwa watawala wa himaya zao. Amin akifa, Mamun atamrithi. Mamun atakuwa na haki ya kumteuwa Kassim kama mrithi wake, akipenda.

Harun Rashid alichukuwa hatua nyingine. aliwataka watoto wake wampe ahadi kwamba wataheshimu mipaka ya kila mmoja na hawatapigana wenyewe kwa wenyewe. Alipata ahadi hii kutoka kwa Amin na Mamun mbele ya Kaaba. Kila mmoja aliandika ahadi yake kukubali madai ya mwingine katika mwaka wa 186 A.H.

Katika mwaka wa 193 A.H. Harun alikufa kijijini Sanabad, Tusi. Alikuwa na miaka 48 alitawala kwa muda wa miaka 23 na miezi sita.

AMIN NA MAMUN WASHIKA MAKOO WENYEWE KWA WENYEWE MWAKA WA  195-198 A.H.

Kama ilivyopangwa na Harun Rashid, Amin na Mamun wakawa watawala wa himaya zao. Lakini Amin alikuwa hakufurahia mpango huu. Akishawishiwa na mshauri wake mkuu, Fazi bin Rabiy, alichukuwa hatua za kijeshi dhidi ya Mamun. Mamun alikuwa dhaifu lakini alikuwa mtawala mwenye uwezo na alikuwa na washauri waaminifu na wenye busara kama vile Fazi Bil Sahil. Vile vile bahati njema ilikuwa upande wake. Baada ya kupigana na ndugu yake kwa muda wa miaka minne, alimshinda Amin katika mwaka wa 198 A.H. Amin alikuwa na Baghdad ikaangukia mikononi mwa Mamun ambaye alitambuliwa kama mtawala pekee wa kile kiichoachwa katika himaya ya baba yake. Katika kipindi cha miaka hii watakati watoto wawili wa Harun Rashid walipokuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe, Imam Ridha (a.s) alipata fursa ya Kuhubiri Uislam kwa Uhuru. Msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) mjini Madina kwa mara nyingine tena ukuwa ni kituo cha elimu cha kufundishia. Kwa baadhi ya Mahesabu, darasa za Imam Ridha (a.s) zilikuwa zikihudhuriwa takribani na wanafunzi 18,000. Sifa yake ilienea katika himaya hii na watu kutoka himaya nyingine zote na nje walikuja Madina kufaidika na ujuzi wake na kujifundisha.

MAMUN AMWITA IMAM RIDHA (A.S) KWENDA KHORASAN IRAN.

Ingawa Mamun amekuwa mtawala wa himaya yote ya Kiislam baada ya kushindwa na kufariki kwa Amin, alikuwa katika hali dhaifu sana. Vita imeiacha tupu hazina yake na jeshi lake kudhoofika. Alikuwa anahitajika kutumia pesa nyingi kujenga upya sehemu kama Baghdad ambayo imeharibiwa vibaya na vita.

Maadui zake wakaichukulia hali hii ya udhaifu kama fursa kwao. Kulikuwa na maasi mbalimbali katika maeneo ya mbali ya himaya hii.

Kwa mfano, Ibn Taba-Taba aliasi dhidi ya serikali katika mwaka wa 199 A.H. na kufa ikawa haiko tena katika mikono ya Mamun. Vilevile Hijazi iliangukia mikononi mwa mtoto wa Imam Jafar Sadiq (a.s).

Zingatia kwamba wengi wa viongozi hawa wa maasi ni wenye kuwahumia Ahlul-Bayt (a.s). Baadhi yao walikuwa 'SADAT'. Ili kuzima upinzani huu dhidi yake, Mamun alikuja na wazo la kijanja. Aligeukia kwa Imam Ridha (a.s) na akaahidi kumuweka kwenye kiti cha Ufalme na kumfanya Khalifa. Sababu aliyoitoa Mamun kuelezea hatua hii ya kushangaza ilikuwa hivi: Wakati alipokuwa anapigana na Amin alikuwa dhaifu sana kiasi kwamba alikuwa na hakika kuwa atashindwa vita hivi. Hivyo aliweka ahadi kwa Allah kwamba kama yeye (Mamun) akiwa mshindi dhidi ya Amin, atautoa ufalme huu na kumpa Imam Ridha (a.s).
Kwa vile Allah amempa ushindi dhidi ya Amin, alitaka sasa kutekeleza ahadi yake.
Imam Ridha (a.s) alijua sababu iliyojificha kwa ajili ya kupewa mamlaka haya. Kwa upole, lakini kwa msimamo imara alikataa zawadi hii. Lakini Mamun alikataa kuikubali 'Hapana' kwa ajili ya swali. Mwaka 201 A.H. alituma jeshi lake kwenda Madina kumrudisha Imam Marv Iran hata ikiwa kwa nguvu. ikiwa lazima. Kamanda wa jeshi alikuwa Rajaa bin Abdul Zahak. Kwa hiyo Imam Ridha (a.s) akawa hana hiari bali kuifanya safari hiyo kwenda Iran. Kabla ya kuondoka aliita familia yake na jamaa zake na akawaaga, akiwambia kwamba hatakuwa na uwezo kamwe wa kurudi tena Madina akiwa hai. Kwa hiyo hii ilikuwa ni kuagana kwao kwa mara ya mwisho.

Njia ya mkato na yenye kufaa kwenda Iran ilikuwa kupitia Kufa mpaka Karman Shah na Qum. Hata hivyo, njia hii inapitia maeneo ambayo yanayokaliwa na watu wenye urafiki na Ahlul-Bayt (a.s). Mamun aliogopa kwamba kama Imam Ridha (a.s) atapitia maeneo haya, wale wenye huruma naye wanaweza kukasirika na kushawishika kufanya uasi dhidi ya serikali. Kwa hiyo Imam Ridha (a.s) alichukuliwa kupitia njia ya mbali wakipitia maeneo ambayo yalikuwa yamekaliwa na watu ambao imma walikuwa hawana habari na ukubwa wa Imam Ridha (a.s) au ambao ni maadui wa Imam Ridha (a.s). Imam Ridha (a.s) alifanya asafiri mpaka Kufa na kutoka huko mpaka Basra na kisha mpaka Marv (Iran) kupitia Ahwza, Shirazi na Naishapur. Licha ya tahadhari hii, Imam Ridha (a.s) alikuwa na mvuto mkubwa sana kwa watu aliokutana nao njiani.
Kwa mfano, wakati Imam Ridha (a.s) alipokuwa katika sehemu inayoitwa Nashapur (Iran), maelfu ya watu walikuja kumlaki na kukutana naye. Walimtaka awasomee Hadithi yoyote ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w).

BAADHI YA HADITHI ZA IMAM RIDHA (A.S):

Imam alisema:
1- Usijiepushe kutumia manukato. Kama ikiwezekana weka manukato kila siku. Vinginevyo weka kila baada ya siku tatu. Kama huwezi kufanya hivyo, basi angalau kila siku ya Ijumaa

2- Kama ukipata sifa yoyote nzuri, usijifaharishe nayo. Bali, muombe Allah kwamba akuwezeshe kuendelea kuifaidi na kwamba aifanye kamili kwa ajili yako.

3- Tunasahau kwamba maisha haya ni ya muda na kutegemea kuishi kwa muda mrefu sana. Ukweli ni kwamba Kifo kitamaliza mategemeo yetu yote ya muda mrefu. Usiache tamaa zako zisizo na maana zikufanye wewe kuwa na fahari. Ishi maisha ya heshima na usiwe na mengi ya hali ya juu. Maisha katika ulimwenguni huu ni kama kivuli kinachopita, na msafiri. Msafiri anapumzika chini ya kivuli na kisha huondoka.

4- Watu hulaumu muda kwa shida zao zote. Ukweli ni kwamba hakuna kosa lolote katika muda. Tatizo tunalo sisi wenyewe sio muda. Kama muda ungeongea, ungetuambia udhaifu wetu wote na hivyo sisi wenyewe kutahayari

5- Imam Ridha anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwamba alisema: Masharti ambayo humfanya mtu kuwa Muumini wa kweli ni: kukubalika kwake kwa maneno, imani yake ya moyo na utendaji wake wa mahitaji ya imani.

IMAM RIDHA (A.S) AKATAA KUWA MTAWALA:

Wakati akiwa Iran, Imam Ridha (a.s) alipewa rasmi uflame na Mamun. Imam Ridha (a.s) alikataa kabisa kukubali. Hoja yake ilikuwa: Kama Mamun aliteuliwa kimungu kama Khalifa, hana haki ya kumpa mtu yeyote uflame wake. Kama kwa upande mwengine, hakuteuliwa kimungu kama khalifa, basi ufalme huo sio wake na atawezaje kumpa mtu yeyote kitu kisichokuwa chake?

Hapa tena Mamun akaamuru akubali kuvishwa taji la ufalme (Wali Ahad) vinginevyo atauliwa. Imam Ridha (a.s) akakubali lakini kwa masharti yafuatayo:-

1- Hatajihusisha katika masuala yoyote ya dola.

2- Hatashiriki katika kuteuwa au kumuachisha mtu yeyote katika kazi ya serikali.

Atatoa ushauri tu pale ambapo ushauri wake kwa mahususi utahitajika.
Mamun akakubali. Kwa hiyo, Imam Ridha (a.s) alitangazwa kama mfalme mteule wa Himaya ya Waislam aliyevishwa taji kwenye sherehe kubwa tarehe 1 Ramadhani 201 A.H.

Imam Ridha (a.s) alijua njama hii nyuma ya hatua hii. Kwa mfano, katika sherehe hiyo kubwa ya kumtangaza Imam Ridha (a.s) kama mfalme aliyevishwa taji, mmoja wa wafuasi wake alikuwa amefurahi sana, Imam Ridha (a.s) akamuonya asiwe mwenye furaha kiasi hicho kwani matokeo ya sherehe hiyo yatakuwa mabay kwa Imam Ridha (a.s).

Imam Ridha (a.s) kamwe hakufurai kwa kuvishwa taji la ufalme. Alikuwa akiongea kuhusu siku zake za furaha wakati alipokuwa Madina ambako alikuwa akitembea kwenye kichochoro vya mjini Madina juu ya mgongo wa mnyama wake huku akiwahudumia masikini wa Madina kama vile walikuwa sehemu ya familia yake.

Ni kiasi gani Imam Ridha (a.s) hakuwa ni mwenye furaha hata kuikubali nafasi hii ya mrithi wa ufalme, hili huelezwa na mtumishi wa Imam, Yasi ambaye alimuona Imam Ridha (a.s) akinyoosha mikono yake mbinguni na kuoma: " Ee Mola wangu! Unajua kwamba nimelazimishwa kukubali cheo hiki (Waliahad). Hivyo usinichukue mimi mwenye kuwajibika kama ambavyo hukumfanya mwenye kuwajibika mtumishi wako Mtume Yusuf kwa kufanya kazi katika serikali ya Misr."

Ili kuthibitisha kwamba Imam Ridha (a.s) alikuwa wa pili katika msitari wa ufalme, Mamun alifanya yafuatayo:-

1- Aliita mkutano wa maofisa na watu watukufu na akawataka wale kiapo cha utii kwa Imam Ridha (a.s). Kusema kweli, wa kwanza kula kiapo chake cha utii alikuwa ni mtoto wa Mamun Abbas.

2- Alichapisha Sarafu zenye jina lake na jina la Imam Ridha (a.s).

3- Aliamuru jina la Imam litajwe katika hutuba za Ijumaa kama mrithi wa Khalifa.

4- Ili kusheherekea tukio hilo, Mamun alitoa kama zawadi maelfu ya Dinar. Washairi walialikwa kumtukuza Imam Ridha (a.s) na Imam Ridha (a.s) alialikwa kutoa hutuba kwa ajili ya kusherehekea tukio hilo.

JINSI GANI WATU WALIPOKEA UTEUZI WA IMAM RIDHA (A.S).

Watu wa ukoo wa Bani Abbas walimkasirikia sana Mamun, kwa vile hawakuelewa sababu ya kweli ni kwa nini Mamun amefanya alivyofanya. Walikuwa na husuda na Imam Ridha (a.s), wakifikiri kwamba heshima ya Imam Ridha (a.s) itapanda. Hawakuelewa kwamba Mamun alikuwa anajaribu tu kuokoa ufalme wake akitumia jina la Imam Ridha (a.s).

Baadhi ya wafuasi wa Imam Ridha (a.s) walichukizwa pia. Hawakuelewa ni kwa nini Imam Ridha (a.s) ametaka kushirikiana na Mamun na kuwa mrithi wake wa ufalme. Kitu ambacho hawakuelewa ilikuwa kwamba Imam Ridha (a.s) alikuwa analazimishwa kukubali uteuzi huu na kukataa kwake kungemaanisha kifo cha mara moja katika wakati ambapo ulimwengu wa Kiislam unamuhitaji zaidi.

Kusema kweli, baadhi ya watu walianza kumkosoa mbele yake kwa kuwa sehemu ya serikali. Alitumia mfano wa Mtume Yusuf kuwaelezea ni kwa nini yeye ni sehemu ya serikali. Alisema kwamba kwa mujibu wa Qur'an ni kama Mtume Yusuf alivyotoa huduma yake kwa Azizi (mfalme) wa Misr ili kusaidia watu. Kwa upande mwingine yeye Imam Ridha (a.s), alilazimishwa kufanya kazi kwa ajili ya Mamun ambaye angalau kwa nje alikuwa Mwislam na hivyo akiwa bora kuliko Azizi wa Misr ambaye hakuwa Mwislam kwa hesabu yoyote.

Kumbuka kwamba Imam Ali (a.s) alishiriki katia kamati ya watu sita iliyoteuliwa na Umar bin Khattab ili kumchagua mrithi wake. Pia kumbuka kwamba Imam Ali (a.s) alisaidia mara kwa mara serikali ya Umar na Uthman wakati yeye, kama Imam aliona hili ni muhimu. Katika njia hiyo hiyo, Imam Ridha (a.s) alimusaidi Mamun katika serikali yake wakati alipoona kwamba hili litakuwa na manufaa kwa Waislam.
Kwa kusema kweli, Imam Ridha (a.s) alitoa maelezo mwenyewe. Hili lilitokea wakati mtu mmoja alipomuuliza: "Ewe mtoto wa Mjumbe wa Allah! Ni kitu gani kilichokufanya ukubali na kuhusika katika suala la urithi wa ufalme?" Imam Ridha (a.s) alijibu: "Kitu kile ambacho kilisababisha babu yangu Amirul Muminin kujihusisha katika SHURA."