Bismillahir Rahmanir Rahim.
Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
“Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni Neema yangu na nimeuridhia kwenu Uislamu kuwa ndiyo dini”
(Qur’an. 5:3).
Mashia wanakubaliana kuwa ilishuka hapo Ghadir Khum baada ya Mtume (s.a.w.w) kumsimika Imam Ali bin Abi Talib (a.s) kuwa ni Khalifa wa Waislamu, na hivyo ni riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wa kizazi kitakatifu, na ndiyo maana utawaona (Mashia) wanauhesabu Uimamu kuwa ni miongoni mwa “Misingi ya Dini” (Usulud-Din). Pamoja na kwamba wengi wa wanachuoni wetu wa Kisunni wanaisimulia Aya hii kuwa ilishuka hapo Ghadir Khum baada ya kusimikwa Imam Ali bin Abi Talib nami ninataja miongoni mwao kama mfn:
Taz:Tarikh Dimishq ya ibn Askir J. 2 uk. 75.
Manaqib Ali bin Abi Talib cha Ibn Maghazili As-Shafii uk. 19.
Tarikh Baqhaad cha Al-Khatib Al-Baghdadi J. 8 uk. 290.
Tafsir ibn Kathir J. 2 uk. 14.
Tunasema, pamoja na yote hayo wanachuoni wa Kisunni wamelazimika kuibalisha ayah ii na kuiweka kwenye mnasaba mwingine, na kufanya hayo yote ni kwa ajili kulinda heshima ya viongozi waliopita miongoni mwa Masahaba, vinginevyo kama wangekubali kwamba aya hiyo imeshuka hapo Ghadir Khum na wengekiri kwamba kutawazwa kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ndiyo jambo ambalo kwalo Mwenyezi Mungu aliikamilisha dini na akawatimizia Waislamu kwa jambo hilo neema yake, na pia ungalitoweka Ukhalifa wa Makhalifa watatu ambao walimtangulia Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na ungeporomoka uadifu wa Masahaba na hadithi nyingi zingeyeyuka kama sukari inavyoyeyuka ndani ya chai. Lakini jambo hili haliwezekani na ni jambo zito kwani lahusika na itikadi ya umma mkubwa wenye historia yake na wanachuoni wake na watukufu wake, hivyo basi imeshindikana kwetu sisi kumpinga Bukhari na Muslim ambao wanasimulia ya kwamba aya hiyo ilishuka Ijumaa jioni ya Arafa. Na kwa riwaya hizo za kina Bukhari zile riwaya za mwanzo zinaonekana kuwa ni uzushi wa Kishia na hazina msingi wowote wa usahihi, na kuwashutumu Mashia inakuwa ni bora mno kuliko kuwashutumu Masahaba, kwani Masahaba hawa wamehifadhika kutokana na makosa kwa sababu wao wanaamini kwamba Masahaba ni kama nyota, yeyote mtakayemfuata mtaongoka. Na wala hapana uwekano wa mtu yeyote kuyakosoa matendo yao na maneno yao. Amma hao Mashia wao ni majusi, makafiri, wazandiki, na ni walahidi na muasisi wa madhehebu yao ni Abdallah bin Sabai soma kitabu kiitwacho Abdillah bin Sabai cha Allamah Al-Askari ili ufahamu kwamba huyu Abdallah bin Sabai hakupata kuwepo duniani bali ni katika watu walioumbwa (kuzushwa) na Seif bin Umar At-Tamimi ambaye ni mashuhuri kwa kuzusha na kuweka (yasiyokuweko) na pia soma Kitabu kiitwacho Al-Fitnatul-Kubra’ cha Taha Husain na ukitaka soma Kitabu kiitwacho As-Silatu Baynat-Tasawwuf Wat-Tashayui’ cha Doctor Mustafa Kamil As-Shaybi ili ufahamu kwamba Abdallah bin Sabai huyu asemwaye si mwingine bali na Sayyidna Ammar bin Yasir (r.a) ambaye ni Myahudi aliyesilimu zama za Uthumani bin Affan ili kuwavuruga Waislamu na Uislamu. Kufanya hivyo ni jambo jepi mno ili kuupotosha umma ambao umehelekea juu ya msingi wa kuwatukuza na kuwaheshimu Masahaba (yaani Sahaba yeyote yule japokuwa alimuona Mtume mara moja) basi itawezakana vipi kwetu sisi kuwakinaisha watu kwamba riwaya hizo siyo uzushi wa Kishia bali ni hadithi za Maimamu kumi na wawili ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka kuhusu Uimamu wao, Maimamu ambao serikali za Kiislamu katika karne ya kwanza zilifanikiwa kupandikiza mapenzi na kuwaheshimu Masahaba dhidi ya Imam Ali bin Abi Talib na wanawe juu ya Mimbar na kuwafuatilia Mashia wao kwa kuwauwa na kuwafukuza, na hapo ndipo ilipoanzia chuki na karaha dhidi ya kila Shia kutokana na mambo yaliyosambazwa na vyombo vya Habari katika zama za Muawiyyah lana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni pamoja na itikadi mbaya dhidi ya Shia, na leo hii Mashia wanaitwa kuwa ni kundi la upinzani ili tu kuwatenga na kuwamaliza. Na kwa ajili hiyo tunawakuta hata waandishi na wanahistoria katika zama hizo wakiwaita Mashia kuwa ni Ar-Rawafidhi” (yaani wapinzani) na huwakufurisha na kuwauwa ili tu kujipendekeza kwa watawala. Ulipoanguka utawala wa Banu Umayyah na ukafuatiwa na dola ya Banu Abbas baadhi ya wanahistoria walibadili muelekeo wao, baadhi yao wakaitambua haki ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) hayo ni kwa sababu ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) nafsi zao zilishakamana na Akhlaq yao njema na elimu zao ambazo zilijaa ulimwenguni, na uchamungu wao na utukufu aliowapa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kutokana na mazingira haya wanahistoria hao wakajaribu kufanya uadilifu na ndipo walipomuunganisha Imam Ali bin Abi Talib (a.s) katika Makhalifa waliomtangulia, likini pamoja na hayo hawakuthubutu kuweka wazi haki yake, na ndiyo maana utawaona hawakuandika ndani ya vitabu vyao isipokuwa sehemu ndogo tu ya ubora wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na tena wanatoa zile sifa ambazo hazipingani na Ukhalifa wa waliomtangulia. Baadhi yao wameweka hadithi nyingi zinazohusu ubora wa Abubakar, Umar na Uthman kwa kupitia ulimi wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) mwenyewe ili wapate kukata njia ya Mashia wanaosema kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni bora zaidi. Kwa kupitia uchunguzi wangu nimegundua kwamba umashughuri wa watu na utukufu wao ulikuwa ukipimwa kwa kiwango cha kumchukia Ali bin Abi Talib (a.s), kwani Banu Umayyah na Banu Abbas walikuwa wakimkurubisha na kumtukuza kila yule ambaye alikuwa akimpiga vita Imam Ali bin Abi Talib (a.s) au akisimama dhidi yake kwa upanga au ulimi, ndiyo maana utawaona wanawatukuza baadhi ya Masahaba na kuwatweza wengine. Si hivyo tu bali (Banu Umayya na Banu Abbas) wakiwashaheneza kwa mali nyingi baadhi ya washairi na kuwauwa wengine, na huenda mama Aisha Ummul-Muuminina asingekuwa na hedhi kwa kiwango hicho kwa Masunni lau siyo kumchukia. Mama Aisha alikuwa hawezi kumtaja Imam Ali bin Abi Talib (a.s) jina lake,
Taz: Bukhar J.1 uk.161. J. 7 uk. 18, J. 5 uk. 140.
Na wanahistoria wanasema mama Aisha zilipomfikia khabari za kuuawa kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alisujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu na alisoma mashairi kuhusu tukio hilo lakuuawa kwake Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na kumpiga vita. Na kwa ajili hiyo pia tunawakuta watawala wa Kibanu Abbas wanamtukuza Bukhar na Muslim na Imam Malik kwa sababu wao hawakuthibitisha ubora wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) isipokuwa kidogo bali, tunakuta wazi wazi ndani ya vitabu hivi kwamba Imam Ali bin Abi Talib (a.s) hana ubora wowote ule wala heshima, kwani Bukhar amesimulia ndani ya Sahihi yake katika mlango unaohusu ubora wa Uthman kwamba imepokewa kutoka kwa Ibn Umar amesema, “Katika zama za Mtume sisi tulikuwa atumlinganishi Abubakar na mtu yeyote, kisha akifuatia Umar kisha Uthman halafu tunawaacha Masahaba wa Mtume (s.a.w.) hatumboreshi yeyote baina yao Sahihi Bukhar J 4 uk. 191 na uk. 201, kama ambavyo Bukhar amesimulia ndani ya Sahihi yake J. 4 uk. 195, riwaya inayonasibishwa kwa Muhammad Al-Hanafiyyah amesema: “Nilimwambia baba yangu, ni nani mtu bora baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, Abubakar akasema kisha nani, akasema kisha Umar nikachelea akasema Uthman nikasema kisha wewe akasema, mimi si chochote isipokuwa mtu miongoni mwa Waislamu. Kwa maana hiyo Imam Ali bin Abi Talib (a.s) kwake si chochote bali ni kama watu wengine (soma na ushangae)!! Kama ambavyo katika umma wa Kiislamu kuna makundi mengine kama vile Muutazilah, Khawarij na wengineo miongoni mwa wale wasiosema semi za Mashia. Wote hao Uimamu wa Imam Ali bin Abi Tali (a.s) na baada yake wanawe, unawanyima nafasi ya kuufikia Ukhalifa, kuwatawala Waislamu na kuichezea hatima yao kama walivyofanya Banu Ummayyah na Banu Abbas katika zama za Masahaba na zama za Tabiina (waliofuatia Masahaba) mpaka leo. Kwani watawala wa zama (zote) ambazo walitawala, sawa iwe kwa njia ya kurithi kama vile ufalme na hata marais wamechaguliwa na wananchi wao itikadi hii hawaipendi yaani Muumini kuitakidi Ukhalifa wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), na huwa wanaicheka kabisa fikra hii. Na fikra hii hakuna aisemaye isipokuwa Mashia, na Mashia hawa wanaonekana wamefikia kiwango cha upuuzi na ujinga wa akili na maoni potofu kwa vile wanaitakidi juu ya Uimamu wa Mahdi anayengojewa ambaye ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa kama ambavyo umejazwa dhulma na ujeuri hivi sasa.