MADHUMUNI YA DINI NA FAIDA YA DINI.

Madhumuni ya dini ni nini na faida ya dini ni nini? kwa nini watu wanakubali dini? Je, kuna tofauti yoyote kati ya watu wa dini na watu wasio na dini? Ona faida ya dini. Watu wanaweza kupata faida zaidi bila ya dini pia; watu hukubali dini kwa ajili ya Heshima, Utukufu, Fahari, Hadhi, Pesa na utajiri.
Mtu anapoenda kupata elimu ya dini, baada ya kumaliza masomo yake akirudi Je, atafanya nini? Ata...
kachofanya kazi ama ya Uimamu wa Swala Msikitini au Mhutubu wa dini popote atakapopata ujira mzuri.

Watu hawafanyi Juhudi ya elimu ya dini kwa madhumuni; wanavutiwa na faida zake wanajua kwamba hii inafaida zaidi. Sasa wanaweza kuona kwamba elimu ya dini iko mikononi mwa watu wabinafsi. Wale ambao wameziharibu nchi za Kiislam na dini ni watu wabinafsi. Ni nini tofauti kati ya madhumuni ya dini na faida ya dini? kwa kweli kwetu sisi wengi wetu, Madhumuni ya dini yanaishia tu kwenye malipo
(Thawaab); hali tulivyo ni- fuata ya dini ili upate Thawaab; funga ili upate Thawaab; tekeleza desturi za dini ili upate Thawaab; soma dua upate Thawaab wahudumie Wanadamu wenzio kwa ajili ya kupata Thawaab; kila kitu kwa ajili ya Thawaab;

"Ulimwengu ni Shamba kwa ajili ya Akhera."
Inamaana kwamba ulimwengu huu ni wa Muundo wa Akhera. Chochote utakachopanda hapa ndicho utakachovuna. Sio kweli kwamba hakuna tofauti kati ya mtu wa dini na mtu asiye wa dini. Simba aliyeko porini na yule aliyeko katika varanda la nyumba ya tajiri sio sawa. Kuna tofauti kubwa kati yao. Katika chumba iko ngozi tu ya simba; katika pori ni mnyama pori, mkali. Mtu asiye wa dini ni sawa na simba aliyeko porini wakati ambapo mtu wa dini mbinafsi ni kama simba wa bandia; ni ngozi ya mwanadamu lakini ndani yake mmeshindiliwa nyasi kavu tu.