Fatma Zahra (a.s),alikuwa ni
mbora wa kuwapendelea wengine kuliko nafsi yake huku akimuiga baba yake katika hilo mpaka imekuwa maarufu kuwa alitoa sadaka gauni lake la harusi usiku wakupelekwa kwa mumewe. Maelezo yaliyomo ndani ya Sura Ad-Dahri yanatosha kuthibitisha upendeleo wake na ukarimu wake. Jabri bin Abdullah Al-Answariy amepokea kuwa: Mtume alitusalisha Swala ya Alasiri na baada ya kumaliza alikaa huku kazungukwa na Maswahaba zake, ghafla akatokea mzee wa kiarabu akiwa kijifunga nguo chakavu akiwa dhaifu mwenye uchovu. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akamfuata na kumuuliza habari zake. Mzee akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nina njaa nilishe, sina nguo nivishe na fikiri nipe masurufu.” Mtume akajibu: “ Mimi sina kitu sasa hivi lakini mwonyesha kheri ni sawa na mtenda kheri, hivyo nenda nyumbani kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda na yeye anawapenda, humtanguliza Mwenyezi Mungu kuliko nafsi yake, nenda nyumbani kwa Fatma.” Nyumba ya Fatma ilikuwa imeungana na nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ambayo alikuwa akiitumia kujitenga na wakeze, akamwambia Bilal: “Ewe Bilal simama umpeleke kwa Fatma.” Akaondoka Bedui akiwa na Bilal na alipofika mlangoni kwa Fatma aliita kwa sauti ya juu: “Amani iwe juu yenu enyi kizazi cha Mtume, mapishano ya Malaika, mashukio ya Jibril roho mwaminifu akiwa na ufunuo kutoka kwa Mola wa ulimwengu.” Fatma akasema: “Waa’leykum Salam, ni nani wewe? “ Akasema mimi ni mzee wa Kiarabu ninahisi njaa, sina nguo, na masikini. Nisaidie Mwenyezi Mungu atakurehemu.” Fatma na wao walikuwa katika hali kama hiyo kwani walikuwa na siku tatu hawajakula chochote, huku tangu mwanzo Mtume (s.a.w.w) akiwa anajua hali hiyo. Hivyo Fatma (a.s) akaenda kuchukua tandiko la ngozi ya kondoo ambalo Hassan na Hussein walikuwa wakilalia. Kisha akamwambia: “Chukua ewe mbisha hodi hakika Mwenyezi Mungu atakubadilishia kwa kukupa kilicho bora zaidi ya hiki.” Bedui akasema: “Ewe bint wa Muhammad, nimelalamika kwako kuwa nina njaa kisha wewe unanipa tandiko la ngozi ya Kondoo nitalifanyia nini huku nikiwa na njaa kama hii? “Fatma (a.s) aliposikia maneno haya alichukua mkufu uliokuwa shingoni mwake ambao alipewa zawadi na Fatma bint wa Ami yake Hamza bin Abdul Muttalib, hivyo akauvua na kumpa Bedui kisha akamwambia: “Chukua ukauuze, hakika Mwenyezi Mungu atakubadilishia kwa kukupa kilicho bora zaidi.” Bedui akachukua mkufu na kwenda nao Msikiti wa Mtume (s.a.w.w) huku Mtume akiwa kaketi na Maswahaba zake. Bedui akasema: “Ewe Mtume, Fatma amenipa mkufu huu.” Mtume akamwambia: “Uza mkufu huo.” Jabir anasema: Mtume akalia na kusema: “Itakuwaje Mwenyezi Mungu asikubadilishie kwa kukupa kilicho bora zaidi ilihali mkufu huo kakupa Fatma bint wa Muhammad mbora wa Wanawake wote wa Ulimwengu!” Ammar bin Yasir akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! je unaniruhusu kununua mkufu huu?” Mtu akajibu: “Ununue ewe Ammar kwani laiti makundi mawili (binadamu na majini) yangeshirikiana kuununua basi Mwenyezi Mungu asingeyaadhibu kwa moto.” Ammar akasema: “Ewe Bedui! Unauza mkufu kiasi gani?” Akajibu: “Kwa kipande cha mkate na nyama, kwa nguo ya kiyemeni ambayo itanitosha kujisitiri na kumwabudia Mola wangu na dinari itakayotosha kunifikisha nyumbani kwangu.” Ammar alikuwa amekwishauza fungu lake alilopewa na Mtume (s.a.w.w) kutoka kwenye vita vya Khaybar, hivyo alikuwa hajabakiwa na kitu, ndipo alipomwambia: “Nakupa dinari ishirini, dirhamu mia mbili za fedha, nguo ya kiyemeni na usafiri wangu utakufikisha nyumbani kwako na nitakushibisha kwa kukupa mkate na nyama.” Bedui akasema: “Ewe ndugu! Hakika wewe ni mkarimu mno.” Hapo akaenda naye na kumpa yote aliyomdhamini. Bedui akarudia kwa Mtume (s.a.w.w) na hapo Mtume akamuuliza: “Je, umeshiba na umevaa?” Bedui akajibu: “Hakika nimetosheka.” Mtume (s.a.w.w) akamwambia: “Mlipe Fatma kwa wema wake.” Bedui akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika wewe ni Mola wa tuliyokuzushia na hatuna Mola tunayepasa kumwabudu isipokuwa wewe, na wewe ndiye mtoa riziki kwetu katika kila hali, hivyo ewe Mola, mbariki bint wa Mtume Fatma kwa kumpa neema ambayo hakuwahi mtu yeyote kuiona wala kusikia.” Hapo Mtume (s.a.w.w) akaitikia dua yake na kisha akawageukia Maswahaba na kuwaambia: “Hakika Mwenyezi Mungu ameshampa Fatma hayo hapa duniani kwani: Mimi ndiye baba yake wala hakuna yeyote ulimwenguni mfano wangu, na Ali (a.s) ndiye mumewe na laiti asingeumbwa Ali (a.s) basi milele Fatma asingepata wa kumsitihili, na akampa Hassan na Hussein wala hakuna yeyote ulimwenguni aliyeruzukiwa watoto mfano wao, wao ni mabwana wa Vijana wa wajukuu wa manabii na mabwana wa Vijana wa Peponi.” Mbele yake alikuwepo Mikdad, Ammar na Salman, Mtume (s.a.w.w) akawaambia: “Je, niwaongozee?” Wakajibu: “Ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akasema: “Jibril amenijia akaniambia kuwa: Atakapozikwa Fatma malaika wawili watamuuliza: Ni nani Mola wako?” Atawajibu: “Allah ndio Mola wangu.” Watamuuliza: “Ni nani Nabii wako? “Atasema: “Baba yangu.” “Na ni nani walii wako?” Atajibu: “Ni huyu aliyesimama mdomoni mwa Kaburi langu.” Mtume akasema: “Je, niwaongeze fadhila zake? Hakika Mwenyezi Mungu amemuwekea walinzi kati ya Malaika wanamlinda mbele na nyuma, kushoto na kulia, wako naye katika uhai wake, kifo chake na ndani ya kaburi lake. Wanazidisha kumwombea rehema na amani yeye na baba yake, mume wake na wanae, hivyo atakayenizuru mimi baada ya kifo changu atakuwa kanizuru wakati wa uhai wangu, na atakayemzuru Fatma atakuwa kanizuru mimi, na atakayemzuru Ali bin Abi Talib atakuwa kamzuru Fatma, na atakayewazuru Hassan na Hussein atakuwa kamzuru Ali, na atakayeviziri vizazi vyao wawili hawa atakuwa kawazuru wao wenyewe.” Hapo Ammar akaenda kuupaka mkufu manukato na kuuweka ndani ya kitambaa cha kiyemeni. Alikuwa na mtumwa aliyemnunua kutokana na fungu lake alilopata toka Khaybar, hivyo akampa mtumwa wake ule mkufu na kumwambia: “Chukua mkufu huu umpelekee Mtume na wewe uwe miliki yake.” Mtumwa akauchukua mkufu ule na kumpelekea Mtume (s.a.w.w) na kumwambia aliyoambiwa na Ammar. Mtume akamwambia: “Chukua mkufu huu umpelekee Fatma na wewe uwe miliki yake.” Mtumwa akauchukua mkufu ule na kumpekea Fatma na kumwambia aliyoambiwa na Mtume (s.a.w.w). Hapo Fatma akamuuliza: “Ewe kijana! ni kitu gani kinachokuchekesha?” Akajibu: “Unachekesha ukubwa wa baraka za mkufu huu, kwani umemshibisha mwenye njaa, ukamvisha asiye na nguo, ukamtajirisha fakiri, ukampa uhuru mtumwa na mwisho ukarejea kwa mwenyewe.”