MTUME (S.A.W.W), ATANGAZA KIONGOZI BAADA YAKE.



Mtume (s.a.w.w) baada ya kumaliza 
 ibada yake ya Hijja ya mwisho, alipokuwa akirejea nyumbani, alifika mahala paitwapo Ghadiir Khum. Ilikuwa tarehe kumi na nane mfungo tatu mwaka wa kumi Hijiria, alipofika Ghadii
r Khum njia panda ziendazo Madina, Misri na Iraq. Ikawa dharura juu ya Mtume (s.a.w.w) kutangaza jambo muhimu la atakaeshika uongozi baada yake, Mtume (s.a.w.w) akaunyanyua mkono wa Imam Ali juu akasema kuwaambia Waislamu waliojumuika zaidi ya laki moja kuwa: "Ambae mimi ni Kiongozi wake, basi huyu (Ali) ni Kiongozi wake. Ee Mola! Muunge atakae muunga Ali na mtenge atakaemtenga (Ali)........."
Waislamu wote wakatoa Baia kwa Imam Ali bin Abi Talib (A.S).

Taz: Tarekh Bughdad J.8 Uk. 290

Tafsirul Kabiir J.12 uK. 49
Ihqaaqul Haqqi J.6 Uk. 225-304
Al-Isaba J.1 Uk. 305